C
Alfabeti ya Kilatini (kwa matumizi ya Kiswahili) | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Aa | Bb | Cc | ch | Dd | ||
Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj | |
Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp | |
Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | ||
Ww | Xx | Yy | Zz |
C ni herufi ya tatu katika alfabeti ya Kilatini. Katika matumizi ya Kiswahili kwa kawaida inatokea tu pamoja na "h" kuwa "ch". C peke yake si kawaida katika maneno ya Kiswahili isipokuwa katika majina ya kigeni.
Maana za C
- kati ya vipimo ºC ni kifupi cha sentigredi za halijoto
- katika muziki, C ni noti.
- katika fizikia c ni alama ya mkasi wa nuru (E=mc2).
- kati ya Namba za Kiroma C ni alama ya "mia moja" (100).
- katika Kemia C ni alama ya Kaboni
Historia ya herufi "C"
Kiebrania gimel | Kifinisia gimel | Kigiriki Gamma | Kiitalia cha awali: C | Kilatini C |
---|---|---|---|---|
ג |
Asili ya herufi C ni pamoja na G katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.
Wafinisia walikuwa na gimel iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya ngamia wakitumia alama tu kwa sauti ya "g" na kuiita kwa neno lao kwa ngamia "gimel". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "gamma" bila kujali maana asilia ya "ngamia" ilikuwa sauti tu ya "g".
Waitalia ya kwanza hawakuwa na sauti ya "g" wakatumia alama kwa aina ya "k". Waroma wakaipokea hivyo lakini walikuwa na sauti ya "g" hivyo mwanzoni walitumia "C" kwa sauti zote mbili. Baadaye waliona vema kutofautisha kati ya sauti za "k" na "g" wakaongeza mstari kwenye C kuifanya G. "C" ikabaki kwao kwa kuandika sauti ya "k". Lakini katika lugha ya Kilatini matumizi ya awali bado hukumbkwa katika kifupi cha jina "Gaius" linalofupishwa kwa kuandika "C.".