Harmonize

Msanii wa Tanzania na mjasiriamali wa muziki

Harmonize (kwa jina lake halisi Rajab Abdul Kahali; mara kadhaa hujiita "Konde Boy"; amezaliwa Chitoholi, mkoa wa Mtwara ni mwimbaji na mtunzi wa muziki kutoka Tanzania.

Harmonize
Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwaRajab Abdul Kahali
Pia anajulikana kamaHarmonize
Asili yakeMtwara,Tanzania
Aina ya muzikiBongo Flava,Afro Pop
Kazi yakeMwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi
AlaPiano, sauti
Miaka ya kazi2011–mpaka sasa
StudioKONDE MUSIC WORLDWIDE
Ame/Wameshirikiana naRayvanny, Diamond Platnumz
TovutiTovuti Halisi

Alianza kuvuma kwa kibao chake cha kwanza "Aiyola" (2015), Bado (2016), Matatizo (2016) na baadaye akatoa nyimbo na msanii mwenzie kutoka lebo moja ya WCB (Wasafi Classic Baby) ambaye ni Diamond Platnumz.

Aliamua kuhama WCB na kuanzisha lebo yake Konde Music Worldwide [1].

Kwa ngwaru ni wimbo ambao ulibamba karibia maeneo yote ya Afrika ya Mashariki akatoa kibao kingine kiitwacho inama nyimbo ambayo aliimba na msanii kutoka nje ya Tanzania ambaye anaitwa burna na diamond Platnumz alikuwepo kwenye huo wimbo. Sasa hivi anatamba na kibao kiitwacho Never Give Up, wimbo ambao unaelezea historia ya maisha yake kuanzia alivyo kuwa na maisha magumu sana. Harmonize anasimamiwa na Joel Joseph au kwa jina lingine Mr Puaz. Kwa sasa msanii huyu yuko peke yake baada ya kujitoa WCB pia amekuwa akitoa ngoma kama vile uno ambayo imepata umaarufu mkubwa na kuwa gumzo yani number one on trending. Pia kwa sasa ameachia kazi yake ya pili iitayo kushoto kulia ambayo amesikika akimtaja Diamond ambapo ni kwa mara ya pili.

Maisha ya Awali

Harmonize ana asili ya Mtwara. Alisoma katika shule ya sekondari Mkundi iliyopo mjini Mtwara. Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari, Harmonize alielekea Dar es Salaam ambako alijipatia riziki yake ya kila siku.

Harmonize mwanzoni alibeba maji ili kupata tonge la chakula, pia alikuwa akiuza kahawa kwa wafanyabiashara wengine na wakazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam kabla ya sauti yake kutambulika mitaani. Kisha kuchukuliwa na lebo ya Diamond Platnumz ijulikanayo kama WCB. Kwa sasa ameamua kujiondoa katika lebo hiyo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Alianza kujihusisha na muziki mnamo mwaka 2011 ambapo alitoa nyimbo mbalimbali lakini hazikuweza kupata umaarufu mkubwa mpaka pale ambapo alikutana na Diamond Platinumz mnamo mwaka 2015 na kuanza kufanya muziki pamoja naye.

Harmonize ndiye mwanamuziki aliyetoa albamu yenye nyimbo 18 akiwa amewashirikisha Yemi Alade wa Nigeria na albamu hiyo inaitwa Afro East.

Diskografia

NambariMada ya wimboMwaka
1.Aiyola2015[1]
2.Bado ft Diamond Platnumz2016
3.Matatizo2017
4.Happy Birthday2017
5.Shula2017
6.Sina2017
7.Niambie2017
8.Dont go2017
9.Nishachoka2017
10.Nakupenda2017
11.Kwa ngwaru ft. Diamond platnumz2018
12.Dm chick2018
13.Atarudi2018
14.Paranawe ft. Rayvanny2018
15.Niteke2019
16.Show me what you gat ft. Yemi Alade2019
17.Kainama ft. Diamond Platnumz na Burna boy2019
18.Ndoenda2019
19.Never give up2019

|20.|Mdomo|2021

Tuzo na teuzi

MwakaKazi iliyoteuliwaTuzoMatokeo
2016Bado Ft Diamond PlatnumzWatsUp TV Tuzo la Video Bora zaidi ya Mwimbaji ChipukiziAmeshinda[2]
Yeye MwenyeweAfrican Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) kwa Mwimbaji ChipukiziAmeshinda[3]
African Entertainment Awards (AEAUSA) kwa Msanii Chipukizi Bora zaidiAmeshinda[4]

2022 kilimanjaro Tanzania music arward= best male artist

Tanbihi

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Harmonize kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.