Mchezo

Mchezo ni shughuli iliyopangwa hasa kama burudani na inayotumika pengine kwa lengo la malezi na la afya.[1]

Kuvuta kamba ni mchezo rahisi usiohitaji maandalizi wala vifaa vingi.
Wachezakarata, mchoro wa mwaka 1895, kazi ya Paul Cézanne.

Mchezo ni tofauti na kazi, inayofanyika kwa kawaida ili kupata malipo, na vilevile na sanaa, ambayo inalenga zaidi kutokeza uzuri au ujumbe fulani. Hata hivyo tofauti hizo si wazi kila mara, maana mambo hayo yanaweza kuchanganyikana katika tukio moja, ambalo linapendeza kwa uzuri, linaburudisha, linalea na kuleta malipo papo hapo.

Ushahidi wa kwanza wa michezo ni wa mwaka 2600 hivi KK[2][3] na kwa sasa baadhi yake imeenea duniani kote[4]

Tanbihi

Marejeo

  • Avedon, Elliot; Sutton-Smith, Brian, The Study of Games. (Philadelphia: Wiley, 1971), reprinted Krieger, 1979. ISBN 0-89874-045-2

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: