Mikoa ya Tanzania


Tanzania imegawiwa katika mikoa 31, ikiwemo 26 upande wa bara na 5 upande wa Zanzibar.

Tanzania

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Tanzania



Zanzibar

Nchi zingine · Atlasi

Mikoa ya Tanzania, miji mikuu, eneo na idadi ya wakazi

MkoaMakao
makuu
WilayaEneo
(km2)
Idadi ya
Wakazi[1]
Msimbo wa
posta
Kanda
ArushaArusha734,5162,356,25523xxxKaskazini
Dar es SalaamDar es Salaam51,3935,383,72811xxxPwani
DodomaDodoma741,3113,085,62541xxxKati
GeitaGeita520,0542,977,60830xxxZiwani
IringaIringa535,5031,192,72851xxxNyanda za Juu za Kusini
KageraBukoba839,6272,989,29935xxxZiwani
KataviMpanda345,8431,152,95850xxxNyanda za Juu za Kusini
KigomaKigoma845,0662,470,96747xxxKati
KilimanjaroMoshi813,2091,861,93425xxxKaskazini
LindiLindi667,0001,194,02865xxxPwani
ManyaraBabati647,9131,892,50227xxxKaskazini
MaraMusoma731,1502,372,01531xxxZiwani
MbeyaMbeya760,3502,343,75453xxxNyanda za Juu za Kusini
MorogoroMorogoro770,7993,197,10467xxxPwani
MtwaraMtwara716,7071,634,94763xxxPwani
MwanzaMwanza79,4673,699,87233xxxZiwani
NjombeNjombe621,347889,94659xxxNyanda za Juu za Kusini
Pemba KaskaziniWete2574272,09175xxxZanzibar
Pemba KusiniChake Chake2332271,35074xxxZanzibar
PwaniKibaha732,4072,024,94761xxxPwani
RukwaSumbawanga422,7921,540,51955xxxNyanda za Juu za Kusini
RuvumaSongea566,4771,848,79457xxxNyanda za Juu za Kusini
ShinyangaShinyanga518,9012,241,29937xxxZiwani
SimiyuBariadi525,2122,140,49739xxxZiwani
SingidaSingida649,4372,008,05843xxxKati
SongweVwawa51,344,687Nyanda za Juu za Kusini
TaboraTabora776,1513,391,67945xxxKati
TangaTanga1027,3482,615,59721xxxKaskazini
Unguja KaskaziniMkokotoni2470257,29073xxxZanzibar
Unguja Mjini MagharibiJiji la Zanzibar2230893,16971xxxZanzibar
Unguja KusiniKoani2854195,87372xxxZanzibar

Mikoa hiyo yote imegawanyika tena kwenye wilaya 169. Wilaya zimeganyika katika kata kibao.

Historia ya mikoa

Ugawaji wa nchi wakati wa ukoloni

Utawala wa Kijerumani

Wakati wa ukoloni wa Kijerumani eneo la Tanzania Bara (=Tanganyika) lilikuwa pamoja na Rwanda na Burundi kama Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mwaka 1913 eneo lote liligawiwa kwa mikoa 21 na maeneo matatu ya wawakilishi wakazi. Mikoa 19 ilikuwa chini ya wakuu wa mkoa wa kawaida yaani maafisa raia Wajerumani (jer. Bezirksleiter au Bezirkamtsmann) waliyemwakilisha gavana na mikoa miwili ilikuwa chini ya mamlaka ya kijeshi yaani afisa wa jeshi la kikoloni la schutztruppe.

Mikoa ya kawaida ilikuwa:

Na.MkoaNa.Mkoa
1.Wilhelmstal (Lushoto)11.Langenburg (Tukuyu)
2.Tanga12.Bismarckburg (Kasanga)
3.Pangani13.Ujiji
4.Bagamoyo14.Tabora
5.Morogoro15.Dodoma
6.Dar es Salaam16.Kondoa-Irangi
7.Rufiji17.Moshi
8.Kilwa18.Arusha
9.Lindi19.Mwanza
10.Songea

Mikoa miwili ya Iringa na Mahenge ilikuwa "mikoa ya kijeshi" yaani chini ya usimamizi ya maafisa wakuu wa jeshi la Schutztruppe.

Maeneo ya Bukoba (takriban sawa na Mkoa wa Kagera wa leo), Ruanda na Urundi yaliendelea kutawaliwa na watawala wao wa kienyeji wakiangaliwa na mwakilishi mkazi wa Ujerumani aliyekuwa kama balozi, mshauri mkuu na msimamizi wa watawala hao.

Utawala wa Kiingereza

Tangu mwaka 1918/1919 eneo la Tanganyika lilikuwa eneo la kudhaminiwa kwa Uingereza bila maeneo ya Rwanda (Ruanda) na Burundi (Urundi). Tanganyika ikigawiwa mwaka 1922 kuwa na mikoa ileile ilhali majina ya Kijerumani yalibadilishwa kuwa majina ya kienyeji kama vile [2]:

Arusha, Bagamoyo, Bukoba, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa (si tena mkoa wa kijeshi), Kilwa, Kondoa-Irangi, Lindi, Mahenge (si tena mkoa wa kijeshi), Morogoro, Moshi, Mwanza, Pangani, Rufiji, Rungwe, Songea, Tabora, Tanga, Ufipa (badala ya Bismarckburg), Ujiji na Usambara (badala ya Wilhelmstal).

Katika miaka iliyofuata mfumo huo wa kiutawala ukabadilishwa. Mnamo mwaka 1948 Waingereza walikuwa na majimbo ("provinces") yafuatayo[3]:

Na.JimboIdadi ya wakazi
1.Central (Kati)821,147
2.Eastern (Mashariki)933,120
3.Lake (Ziwani)1,853,719
4.Northern (Kaskazini)592,300
5.Southern (Kusini)917,648
6.Southern Highlands

(Nyanda za Juu za Kusini)

849,995
7.Tanga557,245
8.Western (Magharibi)952,503
Tanganyika yote7,477,677

Mwaka 1961 Jimbo la Mashariki likagawiwa na Dar es Salaam kuwa jimbo la pekee. Ziwa Magharibi ikatengwa na Mkoa wa Ziwani.

Nyakati za uhuru

Majimbo hayo 10 yalirithiwa na nchi huru ya Tanganyika.

Tarehe 26 Aprili 1964 Tanganyika na Zanzibar zikaungana. Tanzania sasa ilikuwa na majimbo 12. Majimbo hayo yalibadilishwa mnamo 1966 kuwa mikoa 20.

Na.JimboIdadi ya WakaziEneo (km²)Makao makuuMikoa ya baadaye
1.Kati886,96294,301DodomaDodoma, Singida
2.Mashariki955,828107,630Dar es SalaamPwani (kisehemu), Morogoro
3.Dar es Salaam128,7421,393Dar es SalaamPwani (kisehemu)
4.Ziwani1,731,794107,711MwanzaMara, Mwanza, Shinyanga (kisehemu)
5.Ziwa Magharibi514,43128,388BukobaZiwa Magharibi
6.Kaskazini772,43485,374ArushaArusha, Kilimanjaro (kisehemu)
7.Kusini1,014,265143,027MtwaraMtwara, Ruvuma
8.Nyanda za Juu za Kusini1,030,269119,253MbeyaIringa, Mbeya (kisehemu)
9.Tanga688,29035,750TangaKilimanjaro (kisehemu), Tanga
10.Magharibi1,062,598203,068TaboraKigoma, Mbeya (kisehemu), Shinyanga (kisehemu), Tabora
11.Zanzibar165,2531,658ZanzibarZanzibar Shambani, Zanzibar Magharibi
12.Pemba133,858984Chake ChakePemba
Majimbo yote9,084,724928,537
  • Mwaka 1967 Zanzibar Shambani (Rural) ikagawiwa kuwa Zanzibar Shambani Kaskazini na Zanzibar Shambani Kusini. Mikoa hiyo iliitwa baadaye Kaskazini Zanzibar na Kusini Zanzibar.
  • 1971 Mkoa wa Rukwa ulianzishwa kutokana na maeneo ya Mbeya na Tabora.
  • 1972 Mkoa wa Lindi ukatengwa na Mtwara.
  • 1974 Mkoa wa Dar es Salaam ukatengwa na Mkoa wa Pwani
  • 1982 Mkoa wa Pemba ukagawiwa kuwa Kaskazini Pemba na Kusini Pemba
  • 1984 Jina la Mkoa wa Ziwa Magharibi likabadilishwa kuwa Mkoa wa Kagera
  • 2002 Mkoa wa Manyara ukatengwa na Arusha,
  • Mwaka 2012 mikoa minne mipya ilianzishwa ambayo ni
    • Mkoa wa Geita, kutoka maeneo ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera
    • Mkoa wa Katavi, awali ilikuwa Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Rukwa
    • Mkoa wa Njombe, kutoka maeneo ya Mkoa wa Iringa (wilaya za Ludewa, Makete na Njombe)
    • Mkoa wa Simiyu, kutoka maeneo ya mikoa ya Shinyanga (Bariadi, Meatu na Maswa) na Mwanza (Busega).
  • Mwaka 2016 ulianzishwa mkoa wa Songwe kwa kumega mkoa wa Mbeya upande wa magharibi.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: