Orodha ya Marais wa Marekani
Katika Katiba ya Marekani, Rais wa Marekani ni Mkuu wa Taifa pamoja na kuwa Mkuu wa Serikali wa nchi hiyo. Kama mkuu wa tawi la utendaji na mkuu wa serikali ya majimbo, rais ndiye mwenye cheo na madaraka makuu zaidi katika nchi ya Marekani.Rais pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Marekani. Kuchaguliwa kwa rais wa Marekani ni kupitia mfumo wa wawakilishi wenye kura (electoral college), ambapo rais huchaguliwa kwa muhula wa miaka minne. Inawezekana pia kwamba rais achaguliwe kupitia katika Nyumba ya Wawakilishi ya Marekani (US House of Representatives), ikiwa kongamano la wajumbe halikuweza kumchagua rais kwa kumpa mgombea mmoa kura nyingi kuliko mwingine yeyote. Kulingana na Katiba ya Marekani, mtu yeyote hawezi kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo zaidi ya mara mbili.[1] Kukitokea kifo, kujiuzulu au kuondelewa mamlakani kwa rais, Makamu wa Rais wa Marekani atachukulia kiti cha rais. Orodha hii inajumulisha tu wale watu ambao waliapishwa kama rais kufuatia kupitishwa ka Katiba ya Marekani hapo 4 Machi 1789.
Kumeapishwa marais 45, na kumekuwa na marais 46, kwa sababu rais Grover Cleveland alihudumu mihula miwili isiyofuatana, na kwa hivi anahesabiwa mara mbili, kama rais nambari 22 na nambari 24. Marais wanne walifariki kawaida wakiwa mamlakani (William Henry Harrison, Zachary Taylor, Warren G. Harding, na Franklin D. Roosevelt), mmoja akajiuzulu (Richard Nixon), na wanne wakauawa (Abraham Lincoln, James A. Garfield, William McKinley, na John F. Kennedy). Rais wa kwanza wa Marekani alikuwa George Washington, aliyeapishwa 1789 bada ya kupigiwa kura na wajumbe wote katika kongamano. William Henry Harrison alihudumu kwa muda wa siku 31 pekee, mwaka 1841, naye Franklin D. Roosevelt akahudumu kwa muda mrefu zaidi kuliko wote, miaka 12. Rais wa sasa ni Joe Biden, aliyeapishwa 20 Januari 2021.
Marais
'*' maana yake, amefariki madarakani
'**' maana yake, amejiuzulu madarakani
Marejeo
Viungo vya Nje
- Whitehouse.gov: The Presidents
- American Heritage People: The Presidents Archived 10 Februari 2006 at the Wayback Machine.
- American Presidents – History Channel
- American Presidents: Life Portraits
- The Hauenstein Center for Presidential Studies – Grand Valley State University
- POTUS: Presidents of the United States – Internet Public Library