Uswidi

nchi katika Ulaya Kaskazini
(Elekezwa kutoka Sweden)

Uswidi (kwa Kiswidi: "Sverige") ni nchi ya Skandinavia katika Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Ufini (Finland) na Norwei.

Uswidi

Jiografia

Nchi imegawiwa katika mikoa mitatu: Norrland katika kaskazini, Svealand katikati na Götaland katika kusini.

Ina pwani ndefu kwenye bahari ya Baltiki. Kuna daraja la kuvukia mlango wa bahari ya Oresund ya kuunganisha Uswidi na Denmark.

Kuna misitu mikubwa sana na maziwa mengi.

Hali ya hewa ya sehemu kubwa ya Uswidi si baridi kutokana na athira ya mkondo wa Ghuba. Kuna tofauti kati ya urefu wa mchana katika miezi ya Mei hadi Julai na giza wakati wa Desemba. Tarehe 21 Juni ni siku ndefu: hakuna giza kabisa na usiku wake Waswidi hufanya sherehe kubwa ya "midsommar" kwa ngoma na dansi kote nchini.

Mji mkuu ni Stockholm, nao unaongoza kwa wingi wa wakazi.

Milima na vilele

Vilele vya juu kwa kila "landskap" ni kama ifuatavyo. Kumbuka kwamba "landskap" katika Uswidi ni sahihi kidogo tu. Basi maoni mengine kuwepo.

LandskapMlimaKimo
BlekingeRävabacken189
BohuslänBjörnerödspiggen222
DalarnaStorvätteshågna1204
DalslandBaljåsen302
GotlandLojsta hed83
GästriklandLustigknopp402
HallandHögalteknall226
HälsinglandGarpkölen671
HärjedalenHelags1797
JämtlandStorsylen1743
LapplandKebnekaise2104
MedelpadMyckelmyrberget577
NorrbottenVitberget594
NärkeTomasbodahöjden298
SkåneSöderåsen212
SmålandTomtabacken377
SödermanlandSkogsbyås124
UpplandTallmossen118
VärmlandGranberget701
VästerbottenÅmliden550
VästergötlandGaltåsen361
VästmanlandFjällberget466
ÅngermanlandTåsjöberget635
ÖlandHögsrum55
ÖstergötlandStenabohöjden328

Wilaya

LänHerufiMji mkuuEneoRamani
Blekinge länKKarlskrona2.947 km²
Dalarnas länWFalun28.196 km²
Gotlands länIVisby3.151 km²
Gävleborgs länXGävle18.200 km²
Hallands länNHalmstad5.462 km²
Jämtlands länZÖstersund49.343 km²
Jönköpings länFJönköping10.495 km²
Kalmar länHKalmar11.219 km²
Kronobergs länGVäxjö8.467 km²
Norrbottens länBDLuleå98.249 km²
Skåne länMMalmö11.035 km²
Stockholms länABStockholm6.519 km²
Södermanlands länDNyköping6.103 km²
Uppsala länCUppsala8.208 km²
Värmlands länSKarlstad17.591 km²
Västerbottens länACUmeå55.190 km²
Västernorrlands länYHärnösand21.685 km²
Västmanlands länUVästerås5.145 km²
Västra Götalands länOGöteborg23.956 km²
Örebro länTÖrebro8.546 km²
Östergötlands länELinköping10.645 km²
Jumla410.977 km²

Historia

Wakazi wa kwanza kujilikana walikuwa makabila ya Kigermanik kama wakazi wote waliowafuata. Huko Roma Tacitus aliandika juu yao mwaka 98 BK.

Kati ya karne ya 8 hadi ya 11 waliitwa mara nyingi "Waviking" wakiogopwa na wenyeji wa Ulaya bara kwa sababu Waviking walivamia mara kwa mara maeneo ya pwani kwa jahazi zao ndogo. Lakini Waviking au Wanormani ni neno la kutaja watu wa Kaskazini waliovamia na kufanya ujambazi kwenye nchi za Ulaya bara si namna jinsi wenyewe walivyojiita.

Nchi na jirani zake mwaka 1219 BK.

Malkia Margarete I wa Udani aliolewa na mfalme wa Norway. Baada ya kifo cha mumewe alitawala nchi zote mbili na baadaye pia Uswidi. Mwaka 1397 wawakilishi wa falme tatu zilikutana katika mji wa Kalmar (Uswidi ya kusini) na kuelewana juu ya "Umoja wa Kalmar" yaliyounganisha nchi zote za Skandinavia chini ya mfalme wa Denmark ilhali kila nchi iliendelea kujitawala. Wakati ule Ufini (Finland) ilikuwa chini ya Uswidi. Iceland na Visiwa vya Faroe ziliingia pia kwa sababu zilikuwa chini ya Norway wakati ule.

Umoja huo uliendela hadi mwaka 1521. Waswidi walianza kuchoka na utawala wa Kidenmark wakaondoka katika umoja huu mwaka 1521 pamoja na Ufini. Lakini Norway iliendela kuwa chini ya Denmark hadi mwaka 1814.

Uswidi ulijiunga na Matengenezo ya Kiprotestanti na kanisa la Kilutheri likawa dini rasmi nchini hadi mwaka 2000. Hivyo Uswidi ikawa kati ya nchi muhimu sana ya Ulutheri.

Uswidi ulistawi na kueneza himaya yake kuanzia karne ya 17 hadi mwanzo wa karne ya 18 kama mojawapo kati ya nchi zenye nguvu zaidi Ulaya.

Baadaye ilirudi nyuma hadi kunyang'anywa kwa Ufini na Warusi (1809).

Kati ya miaka 1814 na 1905 ililazimisha Norwei kukubali mfalme wa Uswidi kama mfalme wa Norwei pia.

Tangu hapo Uswidi umeshika msimamo wa amani na wa kutoshikamana na nchi yoyote.

Kwa sasa Uswidi ni ufalme wa kikatiba yaani Mkuu wa Dola ni mfalme (kwa sasa Carl XVI Gustaf), lakini huyu mfalme anapaswa kufuata sheria ya katiba ya nchi. Utawala umo mikononi mwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Katika karne ya 20 Uswidi umefaulu vizuri kujenga uchumi ili kuondoka katika umaskini na kuwa moja kati ya nchi tajiri za dunia (ikiwa na nafasi ya 8 kwa pato la kichwa).

Nchi ilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 1995 lakini haikukubali pesa ya Euro ikaendelea na Krona ya Uswidi.

Watu

Uswidi ni nchi kubwa yenye wakazi wachache: mwaka 2017 kwa mara ya kwanza wamezidi milioni 10, wengi wao wenye asili ya makabila ya Kijerumani, lakini kwa sasa 32.2% wana damu tofauti au mchanganyiko.

Lugha rasmi ni Kiswidi, ambacho kinafanana sana na Kidani na Kinorwe. Lugha ya pili kati ya tano zilizokubalika kwa makundi madogo ya asili ni Kifini (5%), lakini siku hizi uhamiaji umefanya Kiarabu kiwe na watumiaji wengi zaidi.

Asilimia 89 wanaweza kuongea Kiingereza pia.

Upande wa dini, 57.7% ni Walutheri, lakini kati yao 2% tu wanashiriki ibada ya kila wiki. Waprotestanti wengine ni 275,000, Waorthodoksi wa Mashariki 100,000 na Wakatoliki 92,000.

Waislamu ni kama 600,000, lakini wengi hawashiriki, na 25,000 tu wanafuata swala tano.

Picha

Tazama pia

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Tovuti rasmi
Habari
Biashara
Utalii


Nchi za Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uswidi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.