Vivumishi
Mifano |
---|
|
Kivumishi ni neno/maneno yanayotoa taarifa ya ziada katika nomino. Kivumishi hufanya kazi ya kufafanua/kuelezea zaidi kuhusu nomino ili kupambanua/kuitofautisha nomino husika miongoni mwa nomino nyingine.
Kiwakilishi ni aina ya maneno ambayo husimama kuwakilisha nomino. Kivumishi hutoa taarifa ya ziada kuhusu nomino, kiwakilishi (endapo nomino haipo) au kivumishi chenzake (endapo kuna vivumishi zaidi ya kimoja katika tungo husika).
- Mifano
- Kijana yule ana tabia nzuri
- Majumba kumi yamevunjika
- Mawingu meusi yametanda angani
- Yule mpole amesafiri
- Bata mweupe ni wa jirani
Aina za vivumishi
- Vivumishi vya sifa
- Vivumishi vya idadi pia vya kiasi
- Vivumishi ya kuuliza
- Vivumishi vya kuonesha/Vivumishi vionyeshi/viashiria
- Vivumishi vya kumiliki
- Vivumishi vya -a unganifu
- Vivumishi vya urejeshi
- Vivumishi vya pekee
- Vivumishi vya jina kwa jina/nomino
- Vivumishi visisitizi
Inafanana kabisa na orodha ya viwakilishi, tofauti yake ni hali ya nafsi tu. Yaani, hakuna kivumishi cha nafsi.
Tazama pia
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vivumishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoJohn MagufuliAngkor WatVitendawiliOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoNgeli za nominoKamusi za KiswahiliNguzo tano za UislamuTanzaniaAina za manenoUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaFasihi simuliziShairiKumaUandishi wa ripotiVivumishiKiswahiliAmri KumiPasakaIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)SilabiDiamond PlatnumzInsha ya wasifuMaumivu ya kiunoPasaka ya KikristoMikoa ya TanzaniaAli Hassan MwinyiNew YorkFasihiLughaNahauNominoTarakilishiOrodha ya makabila ya TanzaniaViwakilishiBarua pepeMshororoMadawa ya kulevya