Z
Alfabeti ya Kilatini (kwa matumizi ya Kiswahili) | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Aa | Bb | Cc | ch | Dd | ||
Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj | |
Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp | |
Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | ||
Ww | Xx | Yy | Zz |
Z ni herufi ya mwisho katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Zeta ya alfabeti ya Kigiriki.
Maana za Z
- katika fizikia Z ni alama ya namba atomia inayotaja idadi ya protoni ndani ya kiini atomia.
- Kwa magari Z ni alama ya gari kutoka Zambia.
Historia ya Z
Kisemiti asilia picha ya jambia (silaha) | Kifinisia Zayin | Kigiriki Zeta | Kietruski Z | Kilatini Z |
---|---|---|---|---|
Asili ya herufi Z ni miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.
Wafinisia walikuwa na alama ya "zayin" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya jambia (silaha) wakitumia alama tu kwa sauti ya "dz" na kuiita kwa neno lao kwa silaha hiyo "zayin". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "Zeta" bila kujali maana asilia ya "jambia". Kwao imekuwa sauti tu ya "dz". Katika maendeleo ya alfabeti walinamisha herufi hadi kufikia umbo lake.
Waitalia wa kale kama Waetruski wakapokea herufi kwa umbo lililofanana na umbo asilia. Waroma wakaichukua kutoka hapa kwa sauti ya "ts" lakini baadaye hawakutamka sauti hii na Z ikafutwa katika afabetiy a Kiroma.
Ila tu tangu karne ya 1 KK Waroma walipoanza kutawala Ugiriki na kupokea maneno mengi kutoka lugha ya Kigiriki walichukua tena Z kwa kuandika maneno yenye asili ya Kigiriki wakarithi pia umbo la baadaye.
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Z kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Z kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |