Nenda kwa yaliyomo

Ubelgiji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Koninkrijk België
Royaume de Belgique
Königreich Belgien

Ufalme wa Ubelgiji
Bendera ya UbelgijiNembo ya Ubelgiji
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: Kifaransa: L'union fait la force ;
Kiholanzi: Eendracht maakt macht ;
Kijerumani: Einigkeit macht stark.
(Kiswahili: "Umoja ni nguvu")
Wimbo wa taifa: La Brabançonne (Wimbo la Brabant)
Lokeshen ya Ubelgiji
Mji mkuuBrussels
50°54′ N 4°32′ E
Mji mkubwa nchiniBrussels
Lugha rasmiKiholanzi, Kifaransa, Kijerumani
Serikali
Mfalme
Wazir Mkuu
Ufalme wa kikatiba
Philippe Saxe-Coburg na Gotha
Alexander De Croo
Uhuru
Mapinduzi ya Ubelgiji
1830
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
30,689 km² (ya 136)
0.71
Idadi ya watu
 - Novemba 2022 kadirio
 - [[{{{population_census_year}}}|{{{population_census_year}}}]] sensa
 - Msongamano wa watu
 
11,697,557 (ya 82)
11,515,793[1]

population_census_year = Novemba 2019
376/km² (ya 22)

FedhaEuro (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD.be
Kodi ya simu+32

-


Ubelgiji (België kwa Kiholanzi, Belgique kwa Kifaransa na Belgien kwa Kijerumani) ni ufalme wa Ulaya ya Magharibi. Ni kati ya nchi 6 zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya ambayo baadaye imekuwa Umoja wa Ulaya.

Imepakana na Ufaransa, Uholanzi, Ujerumani na Luxemburg.

Ina pwani kwenye Bahari ya Kaskazini.

Mji mkuu ni Brussels.

Historiahariri chanzo

"Belgii" lilikuwa jina la wakazi wa kale wa kaskazini mwa Gallia, na Gallia Belgica ilikuwa jimbo la Dola la Roma.

Wakati wa Zama za Kati maeneo yake yalikuwa chini ya Dola Takatifu la Kiroma na tangu mwaka 1477 yalitawaliwa na nasaba ya Habsburg. Watawala hao walikuwa Wakatoliki, hivyo walizuia uenezaji wa Matengenezo ya Kiprotestanti.

Hata hivyo mikoa ya kaskazini ilifaulu kwa njia ya vita kujipatia uhuru na kuanzisha Jamhuri ya Nchi za Chini (Uholanzi) tangu mwaka 1648. Mikoa iliyoendelea kuwa Ubelgiji ya baadaye ilibaki chini ya Habsburg hadi Mapinduzi ya Kifaransa na utawala wa Napoleon aliyeiingiza katika Ufaransa.

Baada ya Mkutano wa Vienna wa mwaka 1815 Ubelgiji iliunganishwa pamoja na Uholanzi kuwa sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Nchi za Chini na hapo ilikuwa sehemu ya kusini ya ufalme huo. Tofauti na sehemu za kaskazini, zilizokuwa na Waprotestanti wengi, mikoa ya Ubelgiji ilikaliwa na Wakatoliki. Tena, wenyeji wa mikoa ya kusini kabisa waliongea Kifaransa, na pia katika sehemu nyingine, ambako watu waliongea Kiholanzi, lugha ya Kifaransa ilikuwa lugha iliyopendwa na matabaka ya juu na wasomi.

Tofauti hizo za kiutamaduni zilichangia kati ya watu wa kusini hisia ya kubaguliwa na katika mapinduzi ya 1830 mikoa yao ilijitenga na Ufalme wa Muungano wa Nchi za Chini na kuanzisha ufalme mpya wa Ubelgiji.

Jiografiahariri chanzo

Majimbohariri chanzo

Ubelgiji ni shirikisho la majimbo matatu:

  • Flandria katika kaskazini lenye Waflandria wanaotumia lugha ya Kiholanzi,
  • Wallonia katika kusini lenye Wawallonia wanaotumia Kifaransa na
  • jimbo la mji mkuu wa Brussels lenye lugha zote.[2]

Katika Wallonia kuna pia wilaya ambayo wakazi wanatumia hasa Kijerumani ambacho ni lugha ya tatu ya kitaifa.[3][4]

Ushindani kama si chuki kati ya makundi hayo ndilo tatizo kuu la nchi.[5][6]

Watuhariri chanzo

Wenyeji (67.3%) wanatofautiana hasa kutokana na lugha: 59% wanaongea hasa Kiholanzi, 40% Kifaransa na 1% Kijerumani.

Wahamiaji wanaongea lugha mama zao: Kiarabu (3%), Kiitalia (2%), Kituruki (1%) n.k.

Kiingereza kinajulikana na 38% za wakazi.

Wakazi wengi ni Wakristo (63.7%), hasa wa Kanisa Katoliki (60.6%), lakini 5% tu wanashiriki ibada za kila wiki; Wakristo wengine ni Waprotestanti (2.1%) na Waorthodoksi (1.6%). Waislamu ni 7.4%. Asilimia 28 hawana dini yoyote.

Tazama piahariri chanzo

Tanbihihariri chanzo

Marejeohariri chanzo

Katika wavuti
Vitabu

Viungo vya njehariri chanzo

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla


Nchi za Umoja wa UlayaBendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ubelgiji kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
🔥 Top keywords: Main PageSpecial:SearchWikipedia:Featured picturesYasukeHarrison ButkerRobert FicoBridgertonCleopatraDeaths in 2024Joyce VincentXXXTentacionHank AdamsIt Ends with UsYouTubeNew Caledonia2024 Indian general electionHeeramandiDarren DutchyshenSlovakiaKingdom of the Planet of the ApesAttempted assassination of Robert FicoLawrence WongBaby ReindeerXXX: Return of Xander CageThelma HoustonFuriosa: A Mad Max SagaMegalopolis (film)Richard GaddKepler's SupernovaWicked (musical)Sunil ChhetriXXX (2002 film)Ashley MadisonAnya Taylor-JoyPlanet of the ApesNava MauYoung SheldonPortal:Current eventsX-Men '97