Eneo lake ni km² 302,072.84 ambalo lina wakazi 59,236,213 (31-12-2020): ni nchi ya 23 duniani kwa wingi wa watu, lakini ya 8 au 9 kwa uchumi. Mtu anayetokea katika nchi hii ya Italia kwa Kiswahili huitwa Mwitalia.
Milima ya Appennini inaunda uti wa mgongo wake, wakati ile ya Alpi, ambayo ni mirefu zaidi, inaunda kwa kiasi kikubwa mpaka kati ya Italia na nchi nyingine za Ulaya.
Mlima mrefu zaidi, ukiwa na mita 4,810 juu ya usawa wa bahari, unaitwa Monte Bianco (Mlima Mweupe) na uko mpakani kwa Ufaransa.
Visiwa viwili vikubwa vya Sisilia na Sardinia ni sehemu za Italia pamoja na visiwa vingi vidogovidogo, vile vya Pelagie vikiwa upande wa Afrika.
Italia ina volkeno 14, ambazo 4 kati yake ziko hai: ile ndefu zaidi kuliko zote za Ulaya (mita 3,329) inaitwa Etna na iko mashariki mwa Sisilia. Italia inaongoza Ulaya kwa wingi wa matetemeko ya ardhi.
Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957 ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa pesa ya pamoja (Euro).
Maendeleo
Italia ni kati ya nchi zilizoendelea, ikiwa na nafasi ya nane kwa nguvu ya uchumiduniani, hivyo ni mwanachama wa G7, G8 na G20.
Sanaa na utalii
Italia ndiyo nchi inayongoza duniani kwa kuwa na mahali pengi (51) pa kimaumbile na pa kihistoria palipoingizwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".
Kwa sababu hiyo pia inashika nafasi ya 5 kati ya nchi zote zilizo lengo la utalii.
Watu
Wananchi wana sifa za pekee kati ya Wazungu wote, hata upande wa DNA, kutokana na jiografia na historia ya rasi.
Ni kati ya nchi ambamo watu wanatarajiwa kuishi miaka mingi zaidi, lakini pia ni kati ya nchi ambapo uzazi ni mdogo zaidi: wanaokufa ni wengi kuliko wanaozaliwa.
Kutokana na umati wa Waitalia waliohama nchi hiyo karne za nyuma, sasa zaidi ya watu milioni 60 nje ya Italia wana asili ya nchi hiyo, mbali na raia zaidi ya milioni 4 wanaoishi nje.
Lugha rasmi ni Kiitalia, inayotegemea zaidi lahaja za Italia ya Kati, lakini siku hizi inatumiwa na wananchi walio wengi hata katika mikoa mingine, ambayo kwa jumla ni 20.
Italy - Eyewitness Travel Guides. DK. 2005. ISBN 1-4053-0781-1.
Northern Italy - Insight Guides. APA Publications. 2004. ISBN 981-234-903-0.
Hacken, Richard. "History of Italy: Primary Documents". EuroDocs: Harold B. Lee Library: Brigham Young University. Iliwekwa mnamo 6 Machi 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
"Italy History – Italian History Index" (kwa Italian na English). European University Institute, The World Wide Web Virtual Library. 1995–2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-15. Iliwekwa mnamo 6 Machi 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Italia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.