Waraka wa kwanza kwa Wathesaloniki

(Elekezwa kutoka 1Thes)
Agano Jipya

Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike ni kitabu cha Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Ni barua iliyoandikwa na Paulo wa Tarso kwa Wakristo wa mji wa Thesaloniki katika Ugiriki ya Kale.

Ukurasa wa kwanza wa waraka huu katika gombo "Minuscule 699".

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Muda wa uandishi

Barua hiyo ni andiko la kwanza la Agano Jipya katika Biblia kwa kuwa ni wa mwaka 50 au 51.

Mazingira

Paulo alikuwa amelazimika kukimbia Thesalonike baada ya wiki 3 tu za utume, hivyo aliogopa kwamba huenda dhuluma zikawakatisha wanafunzi wake tamaa. Kumbe, akina Timotheo walipofika Korintho toka Thesaloniki, walimpa Mtume Paulo ripoti kuhusu hali ya Kanisa la kule na kumuondolea wasiwasi: dhuluma zilikuwa zikiendelea lakini Wakristo wachanga wa huko wako imara katika imani yao mpya, isipokuwa hawaelewi vizuri mambo fulanifulani, hasa kuhusu vikomo vya binadamu.

Hapo Paulo akawaandikia kwa furaha barua tuliyonayo mpaka leo ili kuwahimiza na kuwaelimisha zaidi: haina mafundisho mazito isipokuwa kuhusu mambo ya mwisho (hali ya marehemu na ujio wa pili wa Bwana).

Ni barua tulivu na ya kirafiki, ingawa inatoa maonyo upande wa maadili (1Thes 1:1-3:13; 4:13-17; 5:1-11; 5:16-28).

Mpangilio

Mpangilio wa barua ni uleule wa zile zitakazofuata: baada ya salamu na shukrani kwa Mungu, yanafuata mafundisho ya imani, halafu maadili, na hatimaye salamu nyingine.

Viungo vya nje

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:

Tafsiri ya Kiswahili

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili

Mengineyo

Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa kwanza kwa Wathesaloniki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.