Aina za maneno

Aina za maneno ni dhana au maana ya neno/maneno. Pia aina za maneno huhusisha mgawanyo wa maneno hayo kulingana na matumizi yake.

Kwanza neno ni umbo lenye maana ambalo lina nafasi pande mbili. Neno ni silabi au mkusanyo wa silabi wenye kubeba au kuleta maana fulani.

Aina za maneno

  1. Nomino (alama yake kiisimu ni: 'N')
  2. Viwakilishi (alama yake kiisimu ni: 'W')
  3. Vivumishi (alama yake kiisimu ni: 'V')
  4. Vitenzi (alama yake kiisimu ni: 'T')
  5. Vielezi (alama yake kiisimu ni: 'E')
  6. Viunganishi (alama yake kiisimu ni: 'U')
  7. Vihisishi au Viingizi (alama yake kiisimu ni: 'I')
  8. Vihusishi (alama yake kiisimu ni 'H')

Nomino

Nomino hufanya kazi ya kutaja jina la mtu, kitu au mahali. Kwa mfano: baba, Tanzania, ugonjwa n.k.

Aina za nomino

Kuna aina nne za nomino:

  • 1. nomino za kawaida. Kwa mfano: baba, mama
  • 2. nomino za kipekee. Kwa mfano: Elisha, Angela, Naomi, Christopher
  • 3. nomino za jamii. Kwa mfano: mkutano
  • 4. nomino za dhahania. Kwa mfano: malaika

Viwakilishi

Viwakilishi ufanya kazi ya kusimama badala ya jina au nomino.

Aina za viakilishi

Kuna aina tisa za viwakilishi:

  • 1. viwakilishi vya nafsi. Kwa mfano: mimi
  • 2. viwakilishi vya kuonesha. Kwa mfano: wale
  • 3. viwakilishi vya kumiliki. Kwa mfano: wangu
  • 4. viwakilishi vya idadi. Kwa mfano: wachache
  • 5. viwakilishi vya kuuliza. Kwa mfano: yupi
  • 6. viwakilishi vya kipekee. Kwa mfano: mwenyewe
  • 7. viwakilishi vya a-unganifu. Kwa mfano: la baba
  • 8. viwakilishi vya sifa. Kwa mfano: mfupi
  • 9. viwakilishi vya amba\urejeshi. Kwa mfano: ambalo

Tazama pia

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aina za maneno kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.