Encyclopedia Iranica

Encyclopædia Iranica ni kamusi elezo ya kitaalamu kuhusu historia, utamaduni, na ustaarabu wa watu wa Iran.

Ilianzishwa mwaka 1973 na profesa Ehsan Yarshater ikisimamishwa na taasisi ya Center for Iranian Studies kwenye Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York.

Kamusi elezi hiyo inalenga kukusanya elimu ya kitaaluma kuhusu Iran wa leo lakini pia kuhusu maeneo yote yaliyokuwa sehemu za dunia ya Kiajemi katika historia. na uhusiano baina ya Uajemi na tamaduni nyingine kama vile China na Ulaya.[1] [2] Mradi unapanga kuchapisha jumla ya majuzuu 45 lakini tangu mwanzo maudhui yote inapatikana pia katika intaneti kupitia tovuti iranicaonline.org.

Marejeo

Viungo vya nje