Kundi

Kundi ni idadi ya watu au vitu vilivyopo, vimekusanyika, au vinavyowekwa pamoja. Neno hilo limekuwa likitumika mara nyingi kuonyesha mkusanyiko wa watu, wanyama, ndege wa angani au wadudu. ambapo mkusanyiko huo hutokana ana kuwepo kwa kufanana kwa maana ya tabia au muonekano wao.

Kundi la watu

Baadhi ya wanakundi la wikipedia Tanzania

Mara kwa mara makundi ya watu huhusisha kuwepo kwa jambo fulani kati ya wahusika ambao wamekutana katika kundi hilo. Kwa mfano kuwepo kwa majadiliano juu ya jambo fulani kati yao au katika harakati za kutatua jambo fulani kati yao.

Kuna aina tatu za makundi ya watu:

  • Kundi la kijamii: ni kikundi cha watu wawili au zaidi ambao hufanya shughuli zao kwa ushirikiano.
  • Kundi la kikabila: ni kikundi cha watu ambao wanauheshimu, kuufuata na kuutekeleza utamaduni wao.
  • Shirika: ni chombo kilicho na lengo la pamoja na kinatokana na mazingira ya nje.

Kundi la wanyama

  • Hebivora: ni wanyama walao majani.
  • Kanivora: ni wanyama walao nyama.
  • Omnivora: ni wanyama walao nyama na majani.

Kundi la ndege wa angani

Mara nyingi kundi la ndege wa angani huwa linakuwepo kutokana na kufanana kwa ndege husika, tabia za ndege husika. Kwa mfano ndege wanaoishi pembezoni mwa ziwa au bahari huwa wanakaa au kusafiri katika makundi mbalimbali.

Kundi la wadudu

Katika kundi hili la wadudu wapo wadudu wa aina tofauti tofauti, wapo wadudu watambaao pia wapo wadudu warukao angani. Katika hili pia kundi la wadudu huwepo kwa dhana ya kufanana kwao au hata kutokana na tabia zao. Wapo wadudu wanaoishi katika miti pia wapo wadudu wanaokaa ardhini.

Picha