Mauzo

Mauzo ni shughuli inayohusiana na kuuza au kiasi cha bidhaa au huduma zinazouzwa katika muda fulani.

Mhudumu katika kituo cha mafuta aikijaza mafuta kwenye gari la mteja.

Muuzaji humaliza kitendo cha uuzaji baada ya kujibu mwito wa ununuzi. Kuna kupitisha umiliki wa bidhaa na kulipa, ambapo kuna makubaliano ya bei ambayo italipiwa bidhaa ile. Muuzaji ndiye anayefanya tendo lile la uuzaji na uzo lile linaweza kumalizika kabla ya mnunuzi kumaliza kulipa. 

Ufafanuzi

Mtu au shirika linaloonyesha nia ya kupata bidhaa ya thamani inayotolewa linajulikana kama mnunuzi au mteja mtarajiwa. Kununua na kuuza ni lile tendo la kubadilishana umiliki. Kununua ni kupokea umiliki wa kinachouzwa ilhali kuuza ni kupitisha umiliki kwa mnunuzi baada ya malipo. Muuzaji na mnunuzi huafikiana ili kukamilisha ubadilishaji wa thamani.[1]

Katika mauzo kunaweza kuwa na kujadiliana bei au bei inaweza kuwa isiyobadilika. Sanasana bei ya bidhaa au huduma hukuliwa na haja ya wanunuzi na wingi wake sokoni. Kwa biashara zinazolenga wanunuzi fulani, hasa matajiri, muuzaji anaweza kuiweka bei ya bidhaa bila kuzingatia bei ya ile bidhaa au huduma sokoni.

Mbinu

Mauzo yanaweza kuwa:[2]

  • Ya moja kwa moja
  • Yasiyo ya moja kwa moja
  • Ya kupitia mawakala
  • Ya rejareja
  • Ombi la pendekezo
  • Biashara kwa biashara[3]
  • Ya kielektroniki

Mawakala wa mauzo

Mawakala katika mchakato wa mauzo wanaweza kuwakilisha upande wowote; kwa mfano:

  1. Wakala wa mauzo (kama vile kupitia mauzo shirikishi)
  2. Wakala mnunuzi
  3. Wakala anayewakilisha pande zote mbili
  4. Wakala wa kuangalia shughuli tu
  5. Uwakilishi wa nje wa mambo ya mauzo
  6. Msimamizi wa mauzo wa kutekeleza mikakati ya mauzo na kuratibu idara ya mauzo
  7. Mfanyabiashara muuzaji
  8. Wataalamu wa mauzo mtandaoni

Aina za uuzaji

  1. uso kwa uso (P2P)
  2. uso kwa biashara (P2B)
  3. biashara kwa biashara (B2B)

Aina za mauzo kijiografia

  1. mauzo ya ndani
  2. mauzo ya serikali
  3. mauzo ya nchi
  4. mauzo ya kimataifa[4]

Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mauzo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.