Nahau

Nahau ni semi fupifupi ambazo hutumia lugha/maneno ya kawaida lakini maneno hayo hutoa maana tofauti na ile iliyo kwenye maneno ya awali. Japokuwa nahau hutumia maneno ya kawaida lakini kauli yake ina undani kiasi kwamba kwa wageni wasiofahamu lugha hiyo hawawezi kuelewa maana. Baadhi ya nahau ni kama vile:

  • Amina amevunja ungo
  • Sungura ameaga dunia
  • Lupinga amepata jiko
  • Mussa amevaa miwani
  • Oli hana mkono wa birika
  • Kutonesha kidonda
  • Kukalia kuti kavu
  • Hana mbele wala nyuma
  • Kupiga maji yaani kulewa au kunywa pombe
  • Piga bongo yaani kufikiria au kuwaza sana
  • Mambo yamemwendea mrama yaani kwenda kombo
Mapenzi ni upofu,mfano wa picha ukiwakilisha nahau

Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nahau kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.