Tezi

Tezi ni ogani za mwili zinazotoa dutu za pekee ambazo ni muhimu kwa kazi ya mwili kwa jumla na hasa kwa ogani nyingine. Zinapatikana katika wanyama pamoja na wanadamu na pia katika mimea.

Kimsingi kuna aina mbili za tezi:

  • tezi eksokrini zinazotoa kiowevu chenye kazi ya pekee, kwa mfano tezi za jasho, tezi za mate au tezi za nyongo ya utumbo. Tezi hizi zinaunganishwa na kichirizi ambacho ni njia ya kupeleka kiowevu pale kinapohitajika, kwa mfano mdomoni, kwenye utumbo na kadhalika.
  • tezi endokrini zinazotoa homoni na kuzimwaga katika mzunguko wa damu. Homoni zinazunguka kote mwilini lakini zinaathiri ogani pekee ambazo zina molekuli za kupokea homoni fulani.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tezi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.