Uandishi wa ripoti
Ripoti ni maelezo makamilifu yanayotolewa kama taarifa baada ya kufanya utafiti juu ya mtu, kitu au tukio fulani ambalo limetokea, kwa mfano ajali, kifo, mgomo shuleni na kadhalika.
Ripoti huandikwa kwa madhumuni ya kutoa taarifa ili taarifa hiyo iweze kufanyiwa kazi au walau kuhifadhiwa kama kumbukumbu.
Aina za ripoti
A) Ripoti ya kawaida
Muundo wa ripoti ya kawaida
Ripoti ya kawaida sharti iwe na sehemu kuu nne; sehemu hizo ni:
1. Kichwa cha ripoti
- Ripoti lazima iwe na kichwa cha habari; kichwa hicho huandikwa kwa maelezo machache, kwa herufi kubwa na kupigwa mstari.
- Kichwa huoana na yanayoshughulikiwa. Kwa mfano: RIPOTI YA AJALI MBAYA YA GARIMOSHI
2. Utangulizi wa ripoti
- Utangulizi wa ripoti hueleza kwa muhtasari lengo la ripoti kama ni kutoa taarifa au kumbukumbu.
3. Kiini cha ripoti/mwili
- Kiini cha ripoti kina maelezo yote kuhusiana na tukio lenyewe; sehemu hii huelezea kwa ufasaha mambo yaliyotokea, chanzo chake, ukubwa wake, wahusika, na tukio linalohusika.
- Ufafanuzi huu uwe ni wa ukweli wa kuaminika(si lazima iwe tukio la kweli lakini haistahili kumingisha mtu dhana ya uongo).
- wakati uliopita nanafsi ya tatu hutumika isipokuwa unavyomnukuu myu moja kwa moja.
4. Mwisho wa ripoti
- Hii ni sehemu ya mwisho ya ripoti. Sehemu hii huonyesha mambo makuu mawili:
- maoni/mapendekezo ya mwandishi wa ripoti.
- Lazima sentensi "Ripoti hii imeandaliwa na kuandikwa na:" iwe katika hitimisho, kisha kufuatwa na jina na cheo cha mwandishi pamoja na tarehe.
B) Ripoti rasmi
- Hizi ni ripoti ambazo hufuata utaratibu wa kufanya utafiti kuhusu jambo fulani na kutoa mapendekezo.
- Ripoti rasmi huandaliwa na jopo/tume/kamati teule baada ya kufanya uchunguzi wa kina.
- Mambo yanayoandikwa huhutaji uchunguzi na utafiti k.v. majanga, kashfa mbalimbali kama ufisadi, utafiti wa kielimu n.k
- Hutengwa muda maalum wa kuzikamilisha na kuziwakilisha kwa mtu ambaye aliagiza kuchunguzwa kwa masuala hayo.
Muundo wa ripoti rasmi
1. Kichwa
- Kichwa huonyesha ripoti ni ya kina nani/kamati gani, kuhusu nini, wapi na kipindi kilichohusishwa cha wakati.
- Huandikwa kwa herufi kubwa na kipigwa mstari.
- Kwa mfano: RIPOTI YA WIZARA YA AFYA KUHUSU MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA MIONGONI MWA WANAFUNZI WA SHULE ZA UPILI NCHINI KENYA, MWAKA WA 2018
- Huteuliwa kulingana na mada inayoshughilikiwa.
2. Utangulizi
- Huelezea historia mfupi wa jambo linaloandikiwa ripoti.
- Hujumuisha maelezo kuhusu yaliyotukia na kusababisha haja ya kufanywa utafiti/uchunguzi unaopelekea kuandikwa kwa ripoti.
- Wanajopo wanaweza kutajwa pamoja na vyeo vyao.
- Muda ambao kamati/jopo ilichukua kufanya utafiti huo huandikwa.
- pia unaweza kutaja tarehe na atakayewasilishiwa ripoti hiyo.
3. Mbinu za ukusanyaji data
- Mbinu zilizotumiwa kukusanya data inayowasilishwa unaelezwa hapa.
- Mbinu hizo ni pamoja na:
- Mapelelezi
- Hojaji
- Mahojiano
- Kurejelea ripoti nyingine kuhusu mada huo
- Huandikwa kwa mfululizo.
4. Matokeo/Mwili
- Mwili ya ripoti huweka wazi matokeo ya uchunguzi, utafiti au yaliyoshuhudiwa.
- Huandikwa kwa mada ndogondogo.
- Kila mada huzungumzia jambo/suala moja pekee.
- Maudhui huwasilishwa chini ya mada hizi.
- Ripoti huandikwa kwa nafsi ya tatu, kauli ya kutendewa k.v. Iligunduliwa.....Walichojiwa kuwa.....Kamati iliambiwa kuwa....
- Yote yanayoripotiwa yanafaa kuwa ya kuaminika au yaliyo ya ukweli wa kuaminika.
5. Matatizo
- Matatizo huandikwa kwa baadi ya ripoti.
- Yawe ya kuaminika kulingana na mada inayochunguzwa.
6. Hitimisho
- Jumla kuhusu matokeo na mapendekezo hutolewa.
- Kisha kuna jina la mwandishi, cheo chake, sahihi na tarehe.
7. Mapendekezo
- Ushari ambao hutolewa ili kutatua shida ambayo inatokea.
- Hutolewa na wanakamati au na anayeandika ripoti kutokana na uchunguzi uliofanywa.
- Hupendekeza suluhisho zitazochukuliwa ili kudhibiti/kurekebisha hali fulani.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uandishi wa ripoti kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaFaili:Celliphine Chespol Tampere 2018.jpgFaili:20090815 Meselech Melkamu.jpgMwanzoTendo la ndoaJoseph ButikuUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaWikipedia:JumuiaKamusi za KiswahiliTanzaniaTakwimuHaki za watotoOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoKumaOrodha ya nchi za AfrikaAina za manenoFasihi simuliziMikoa ya TanzaniaVivumishiKisaweDiamond PlatnumzUandishi wa ripotiMajadiliano ya mtumiaji:Mr Accountable/Archived Agosti 2010ShairiUtamaduniUkimwiKigezo:All system messagesUgonjwa wa moyoJumuiya ya Afrika MasharikiKiswahiliNahauUsafi wa mazingiraOrodha ya makabila ya TanzaniaSitiariLughaShinikizo la juu la damuBarua pepeSentensiOrodha ya Watakatifu Wakristo