Vichekesho

Vichekesho ni maigizo mafupi yenye lengo la kufikisha ujumbe kwa njia ya kufurahisha au kuchekesha hadhira husika. Vichekesho huundwa kwa mpangilio wa maneno ulio na utendekaji ambao hauna kina kuhusu kisa kinachooneshwa - huonesha kisa au jambo bila kulichambua kwa kina.

Rowan Atkinson akiwa kama Mr. Bean.

Vichekesho hutumia wahusika ambao hutumia lugha nyepesi ya picha na tamathali ambazo watazamaji wana uwezo wa kuzitambua. Vichekesho huigizwa kwenye runinga, redioni, shuleni, na kwenye sherehe mbalimbali.

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vichekesho kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.