Akko

Akko (kwa Kiebrania: עַכּוֹ, ʻAkkō; pia: Akka (kwa Kiarabu: عكّا, ʻAkkā[1]; uliwahi kuitwa pia: Tolemais) ni mji wa pwani katika Israeli Kaskazini. Una bandari asili katika Hori ya Haifa.[2]

Akko kutoka juu.

Kutokana na umuhimu wa mahali ulipo, umekaliwa na watu mfululizo tangu zama za Shaba hadi leo,[3] ingawa uliwahi kuangamizwa mara kadhaa.

Wakazi wa sasa ni 48,000 hivi.

Mwaka 58 Mtume Paulo alikaa siku moja na Wakristo wa huko mwishoni mwa safari yake ya tatu ya kimisionari, akielekea Yerusalemu (Mdo 21:7)

Umeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.

Ni pia makao makuu ya dini ya Bahai.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Akko travel guide kutoka Wikisafiri

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Akko kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.