Barakoa ya kinga

Barakoa za kinga hutumiwa kulinda uso au sehemu zake (macho, pua, n.k.) na viungo vya kupumua dhidi ya athira ya hatari.

Tabibu akiwa amevaa barakoa.
Wakazi wa Hong Kong wakiwa na barakoa wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona Covid-19.
Polisi akiwa amevaa barakoa ya kinga dhidi ya hewa chafu barabarani.

Kuna aina mbalimali za barakoa zinazovaliwa kwa shughuli mbalimbali

  • barakoa za kitiba, zinazovaliwa na matabibu wakati wa upasuaji
  • barakoa za kinga dhidi ya maambukizi, zinazovaliwa na watu wakihudumia wagonjwa au wakihofia maambukizi wakati wa mlipuko wa ugonjwa
  • barakoa za kazi zinazovaliwa na mafundi wakati wa kufanya kazi zinazosababisha moshi au vumbi nyingi, kama vile kufuma, kusaga mbao, kufagia
  • barakoa za oksijeni (kwa wagonjwa au kwa zimamoto)
  • barakoa za gesi, zenye filta zinazokinga dhidi ya gesi sumu kwa matumizi ya kijeshi au huduma za ukoaji katika mazingira ya hatari

Barakoa za aina hizo zinaweza kulinda moja kwa moja dhidi ya maumizi kutokana na kupigwa kwa vipande vidogo vinavyorushwa hewani, au gesi au mvuke hatari, au vumbi, au harufu mbaya.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Barakoa ya kinga kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.