Basilika la Mt. Paulo

Basilika la Kipapa la Mt. Paulo Nje ya Kuta ni mojawapo kati ya mabasilika ya zamani na muhimu zaidi ya Roma[1] pamoja na yale ya Mt. Yohane huko Laterano, Mt. Petro huko Vatikano na Mt. Maria huko Eskwilino.

Upande wa mbele wa Basilika-
Mlango mtakatifu.
Mosaiki ya mwaka 1220 ikimuonyesha Kristo kati ya mitume Petro na Paulo, Mtume Andrea na Mwinjili Luka.
Undani wa kanisa.
Ramani ya basilika
Sibori ya Arnolfo di Cambio.
Mt. Paulo Nje ya Kuta.
Nguzo za nje.

Basilika liko katika eneo la Italia[2], lakini Ukulu Mtakatifu unalimiliki kabisa[3]kama ilivyo kwa maeneo ya balozi za nchi ya kigeni.[4]

Basilika lilianzishwa na kaisari Konstantino Mkuu juu ya mahali (cella memoriae) alipozikwa Mtume Paulo baada ya kukatwa kichwa nje ya ngome ya jiji la Roma.[5][6][7][8][9][10]

Baada ya mabadiliko mengi, lilijengwa upya katika karne ya 19 kwa sababu lilikuwa limeteketezwa na moto. Vipimo vyake ni mita 131.66 kwa 65 kwa 29.70, hivyo ni kanisa la pili kwa ukubwa mjini Roma.

Kumbukumbu ya kutabarukiwa kwake inafanyika kila mwaka tarehe 18 Novemba[11].

Tangu mwaka 1980 Basilika hilo liko katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje