Bwana

Bwana ni jina la heshima linalotumika kwa mmoja ambaye ana mamlaka fulani.

Katika dini mbalimbali linatumika kwa Mungu.

Katika tafsiri za Biblia, kuanzia ile ya awali maarufu kama Septuaginta, jina hilo linashika nafasi ya YHWH, kufuatana na desturi ya Wayahudi ya kutotaja jina hilo la fumbo na hivyo kulisoma Adonai (Bwana) wakilikuta katika Biblia.[1]

Tangu awali Wakristo walipokea na kuendeleza desturi hiyo kwa kumkiri Yesu kuwa Bwana. Kadiri ya Mtume Paulo, “hawezi mtu kusema, ‘Yesu ni Bwana’, isipokuwa katika Roho Mtakatifu” (1Kor 12:3) anayemtia imani ya kuwa huyo aliyetupwa na watu wake ametawazwa na Baba juu ya wote.

Katika Uislamu neno la Kiingereza "Lord" linatumika pengine kutafsiri رب, rabb, sifa ya Allah.

Tanbihi


Viungo vya nje