Mungu Baba


Mungu Baba ni nafsi ya kwanza ya Mungu katika imani ya Wakristo (isipokuwa Wasiosadiki Utatu)[1][2].

Katika Uyahudi

Katika Uyahudi Mungu aliitwa pengine Baba kwa jinsi alivyo asili ya uhai na anavyoshughulikia watu wake, hasa Waisraeli, mfalme wao na mafukara, wanaopaswa kumtegemea kama watoto.[3][4][5][6]

Katika Ukristo

Kumbe katika Agano Jipya yeye ni hasa Baba wa Yesu, anayejitambulisha kama Mwana pekee wa Mungu. Nafsi hizo mbili pamoja na Roho Mtakatifu zinasadikiwa kuwa Mungu mmoja tu, asiyegawanyika katu.[7][8][9][8]

Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli tangu mwaka 325 inafafanua kuwa Yesu Kristo "amezaliwa na Baba tangu milele yote", yaani si uzazi uliotokea wakati wowote wala mahali popote duniani. Daima Mungu Baba ni Baba wa Mwana, asingeweza kuwepo bila kumzaa Mwana.

Wakristo wanafurahia kujua na kushirikishwa uhusiano huo wa milele kwa kufanywa na Roho Mtakatifu (Gal 4:4) "wana ndani ya Mwana pekee": ndiyo maana ya kujiita "wana wa kambo" wa Mungu, wakati Yesu ni Mwana asilia.[10][11]

Katika Uislamu

Uislamu unamuamini Mungu kama muumbaji wa ulimwengu wote, lakini hauhimizi kumuita "Baba" kwa kuwa unataka kusisitiza ukuu wake usio na kifani.[12][13][14][15][16]

Tanbihi

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.