Chapanya
Chapanya | ||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Chapanya (Pseudaspis cana) | ||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||
|
Chapanya ni spishi ya nyoka pekee ya jenasi Pseudaspis katika familia Lamprophiidae. Anaitwa jina hili kwa sababu hula panya.
Spishi hii ni mrefu kiasi, kwa wastani m 1-1.3 lakini hadi m 1.8. Kichwa ni kidogo chenye pua fupi na bapa. Waliokomaa wana rangi moja tu: machungwa, kahawia, kijivu au nyeusi. Wachanga wana rangi zilizoiva na mabaka meusi au kahawia.
Chapanya huwinda wagugunaji katika vishimo vyao. Kinyume na jina lake hukamata mafuko hasa. Lakini wachanga hula mijusi.
Nyoka huyu hana sumu. Akitishwa anatoa sauti ya kuchata na kududia mwili na kupiga mdomo ukifunguliwa kabisa. Lakini hang'ati sana.
Picha
- Chapanya mchanga
Marejeo
- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
![]() | Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chapanya kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoShairiJumuiya ya Afrika MasharikiUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaFasihi simuliziNembo ya TanzaniaMshororoMikoa ya TanzaniaVivumishiOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoPentekosteAina za manenoTanzaniaKamusi za KiswahiliMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaOrodha ya makabila ya TanzaniaAfrika Mashariki 1800-1845Orodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUpendo Furaha PenezaMafurikoMisimu (lugha)KumaKisaweSentensiDiamond PlatnumzKamusi ya Kiswahili sanifuKamusiMisemoMaudhuiSimba S.C.Ukwapi na utaoTanganyikaOrodha ya Watakatifu WakristoNgeliLahaja za KiswahiliMaumivu ya kiunoRoho MtakatifuNomino