Damaris

Damaris (kwa Kigiriki: Δάμαρις) alikuwa mwanamke wa Athene katika karne ya 1.

Matendo ya Mitume (17:34) kinamtaja kati ya wale waliomsikiliza Mtume Paulo alipohubiri kwenye Areopago mwaka 50 hivi. Pamoja na Dionysius Mwareopago alisadiki maneno yake [1]

Baadaye tu wengine walianza kudhani alikuwa mke wa Dionysius.[2][3][4][5]

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Oktoba[6] ambayo ni sawa na 16 Oktoba katika kalenda ya Gregori.

Tanbihi

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Damaris kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.