Grand Canyon
Grand Canyon ni korongo maarufu huko Arizona nchini Marekani. Linaundwa na Mto Colorado uliochimba tangu miaka milioni kadhaa bonde lenye kina kirefu katika miamba ya nyanda za juu za Colorado.
Grand Canyon huwa na urefu wa km 446 na upana hadi km 29. Kuna sehemu ambako ina kina cha mita 1830 [1].
Imeandikishwa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO [2] ikiwa pia Hifadhi ya Taifa ya Marekani.
Utalii
Miaka | Wageni [3] |
---|---|
kabla ya Vita Kuu ya Pili | > 100,000 |
1965 | Milioni 1.6 |
2000 | Milioni 4 |
Korongo hilo ni kati ya vivutio vikubwa kwa watalii nchini Marekani. Kila mwaka inatembelewa na wageni milioni kadhaa wanaofika kutoka ndani na nje ya nchi ya Marekani.
Marejeo
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Grand Canyon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoFasihi simuliziAina za manenoShairiVivumishiMikoa ya TanzaniaOrodha ya makabila ya TanzaniaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaLughaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoKamusi za KiswahiliMofimuFasihiNembo ya TanzaniaMawasilianoSentensiMarie AntoinetteKamusiMange KimambiKumaViwakilishiAlama ya uakifishajiKitenziFani (fasihi)TamthiliaVitendawiliNominoKiswahiliMaudhuiSilabiTanzaniaJumuiya ya Afrika MasharikiKisaweVieleziYoung Africans S.C.Kiwakilishi nafsiDiamond Platnumz