K-rupt

Carlton Williams Bongo Juma (15 Novemba 1979 - 29 Novemba 2003) alikuwa msanii wa muziki wa hip hop kutoka mjini Nairobi huko nchini Kenya. Alifahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama K-rupt. Alikuwa akifanyia shughuli zake katika studio ya Ogopa Deejays.[1]

K-rupt
Jina la kuzaliwaCarlton Williams Bongo Juma
Pia anajulikana kamaK-rupt
Amezaliwa1981
Asili yakeNairobi, Kenya
Aina ya muzikiHip hop
Kazi yakeRapa
Miaka ya kazi1999-2003

K-rupt aliuawa na jelaha la pigo moja la risasi akiwa katika basi dogo (matatu) akiwa anatokea Nanyuki akielekea Nakuru. K-rupt alipanda basi hilo kwa lengo la kwenda kufanya tamasha lake huko mjini Nakuru. Wanyang'anyi hao walipanda basi hilo na kutoa agizo kwa dereva asimamishe gari katika eneo la Karuga, kama kilomita saba hivi kutoka kando ya barabara. Mashuhuda walieleza ya kwamba K-rupt, aliyekomea umri wa miaka 24, alikuwa akibishana na majambazi hao ambao pia ndiyo waliomtandika risasi, na kumuua kwa riasi moja tu. Waliutupa mwili wake katika Msitu wa Laikipia kulingana na taarifa ya polisi.[2]

Diskografia

  • "Changamshwa"
  • "Tukawake"
  • "Chacha"
  • "Dada Njoo"
  • "Bamba" (E-Sir feat. Big Pin & K-rupt)

Marejeo