E-Sir

Msanii wa hip hop wa Kenya

Issah Mmari (alifahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama E-Sir; 20 Mei 198116 Machi 2003) alikuwa msanii wa muziki wa hip hop na kapuka kutoka jijini Nairobi huko nchini Kenya.

E-Sir
Jina la kuzaliwaIssah Mmari
Pia anajulikana kamaE-Sir
Amezaliwa1981
Asili yakeSouth C, Nairobi, Kenya
Aina ya muzikiHip hop, Kapuka
Kazi yakeRapa
Miaka ya kazi2001-2003

Alikuwa akifanyia shughuli zake katika studio ya Ogopa DJs ambaye alikuwa maarufu kwa uwezo wake wa kuimba na amri ya lugha ya Kiswahili. Bado yeye huonekana kama muimbaji wa rap bora sana kuwahi kutokea nchini Kenya. Alikuja kujulikana mwaka 2001 na wimbo wakea wa "Jo", wimbo aliufanya katika sambamba na mtindo wa Black Rob katika ngoma yake ya "WHOA." Wimbo huo ulifanya E-Sir's ajulikane katika mziki wa Kenya na aliwekwa katika albamu ya Ogopa Deejays Aliweza kutoa alikwenda albamu yake ya "Nimefika" mwaka wa 2003 ambayo iliweza kufanya vema zaidi. Yeye alishinda katika sehemu 4 kwenye Kisima Music Awards ya mwaka 2003.

E-Sir alikufa kwa ajali ya barabarani tarehe 16 Machi 2003, akiwa na mwenzake Nameless. Alikuwa njiani kutoka mji wa Nakuru alipokuwa amekwenda kupigia upato albamu yake. Mashabiki wake walikuwa na huzuni na mshangao mkubwa baada ya kusikia juu ya msanii huyu shupavu. Hasa hii ni kwa sababu kifo chake kilikuja wakati nyimbo zake zilikuwa zimeanza kufana sana nchini. Nyimbo zilizojulikana zaidi ni kama "Mos Mos," "Boomba Train," "Hamunitishi" na "Leo ni Leo." Kuna wimbo mmmoja uliotokea baada ya kifo chake.Wimbo huo alifanya na Nameless na unaitwa "Maisha".

Ndugu mdogo wa E-sir Habib pia ni msanii na pamoja na Manga wametoa nyimbo kadhaa kama "dunda" na "fever".

Albamu ya nimefika

Nyimbo kwenye Albamu

  • 1.Jobless corner 1 (Skit)
  • 2.Kamata
  • 3.Bamba
  • 4.Moss Moss
  • 5.Saree
  • 6.Jobless Corner 2 (skit)
  • 7.Sweet Kid ulimi twister
  • 8.Hamunitishi
  • 9.Deux Train
  • 10.Leo ni Leo
  • 11.Nimefika 'Jo'
  • 12.Saree
  • 13.Kamaiko (skit)

Tuzo

Alishinda

  • Kisima Music Awards 2003 - Nyimbo ya mwaka ( "Bumba Train") & Mwanaume Mwanamziki wa mwaka, Albamu ya Mwaka ( "Nimefika")

Kuchaguliwa

  • Kora Awards 2003 - Mwanamziki Bora Afrika Mashariki [1]
  • Tanzania Music Awards 2004 - Albamu bora Afrika Mashariki( "Nimefika") [2]

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu E-Sir kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.