Kaunti ya Bungoma

Kaunti ya Bungoma ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Ramani ya Bungoma, Kenya
Bungoma, Kenya

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,670,570 katika eneo la km2 3,023.9, msongamano ukiwa hivyo wa watu 552 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Bungoma.

Utawala

Kaunti ya Bungoma ina maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eeneo bungeKata
BumulaBumula, Khasoko, Kabula, Kimaeti, South Bukusu, Siboti
KabuchaiKabuchai/Chwele, West Nalondo, Bwake/Luuya, Mukuyuni
KanduyiBukembe West, Bukembe East, Kanduyi Mjini, Khalaba, Musikoma, East Sang'alo, Tuuti/Marakaru, West Sang'alo
KimililiKibingei, Kimilili, Maeni, Kamukuywa
Mlima ElgonCheptais, Chesikaki, Chepyuk, Kapkateny, Kaptama, Elgon
SirisiaNamwela, Malakisi/South Kulisuru, Lwandanyi
TongarenMbakalo, Naitiri/Kabuyefwe, Milima, Ndalu/Tabani, Tongaren, Soysambu/Mitua
Webuye MagharibiSitikho, Matulo, Bokoli
Webuye MasharikiMihuu, Ndivisi, Maraka

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]

  • Bumula 215,892
  • Bungoma Central 177,748
  • Bungoma East 114,548
  • Bungoma North 121,317
  • Bungoma South 287,765
  • Cheptais 136,035
  • Kimilili-Bungoma 162,038
  • Mt. Elgon 78,873
  • Bungoma West 119,875
  • Tongaren 100,343
  • Webuye West 152,515
    • Mt. Elgon Forest 3,621

Tazama pia

Tanbihi