Kaunti ya Nakuru

Kaunti ya Nakuru ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Ziwa Nakuru kaunti ya Nakuru

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 2,162,202 katika eneo la km2 7,462.4, msongamano ukiwa hivyo wa watu 290 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Nakuru.

Utawala

Kaunti ya Nakuru ina maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eeneo bungeKata
BahatiDundori, Kabatini, Kiamaina, Lanet/Umoja, Bahati
GilgilGilgil, Elementaita, Mbaruk/Eburu, Malewa West, Murindati
Kuresoi KaskaziniKiptororo, Nyota, Sirikwa, Kamara
Kuresoi KusiniAmalo, Keringet, Kiptagich, Tinet
MoloMariashoni, Elburgon, Turi, Molo
NaivashaBiashara, Hells Gate, Lake View, Maiella, Mai Mahiu, Olkaria, Naivasha East, Viwandani
Nakuru Mjini MagharibiBarut, London, Kaptembwo, Kapkures, Rhoda, Shabaab
Nakuru Mjini MasharikiBiashara, Kivumbini, Flamingo, Menengai, Nakuru East
NjoroMau Narok, Mauche, Kihingo, Nessuit, Lare, Njoro
RongaiMenengai WesSoint, Visoi, Mosop, Solai
SubukiaSubukia, Waseges, Kabazi

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]

  • Gilgil 185,209
  • Kuresoi North 175,074
  • Kuresoi South 155,324
  • Molo 156,732
  • Naivasha 355,383
  • Nakuru East 193,926
  • Nakuru North 218,050
  • Nakuru West 198,661
  • Njoro 238,773
  • Rongai 199,906
  • Subukia 185,164

Tazama pia

Tanbihi