Kaunti ya Narok

Kaunti ya Narok ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Picha ya ramani ikionesha eneo la Kaunti ya Narok, Kenya
Barabara ya Keekorok ya kuelekea Narok

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,157,873 katika eneo la km2 17,950.3, msongamano ukiwa hivyo wa watu 65 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Narok.

Mara Triangle (ambayo ni sehemu ya hifadhi ya Masai Mara) imo katika eneo la Trans-Mara.

Utawala

Kaunti ya Narok imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eneo bungeKata
Emurua DikirrIlkerin, Ololmasani, Mogondo, Kapsasian
KilgorisKilgoris ya Kati, Keyian, Angata Barikoi, Shankoe, Kimintet, Lolgorian
Narok MagharibiIlmotok, Mara, Siana, Naikarra
Narok MasharikiMosiro, Ildamat, Keekonyokie, Suswa
Narok KaskaziniOlpusimoro, Olokurto, Narok Mjini, Nkareta'Olorropil, Melili
Narok KusiniMajimoto/Naroos, Ulolulung'a, Melelo, Loita, Sogoo, Sagamian

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]

  • Narok East 115,323
  • Narok North 251,862
  • Narok South 238,472
  • Narok West 195,287
  • Trans Mara East 111,183
  • Trans Mara West 245,714
    • Mau Forest 32

Tazama pia

Tanbihi