Kitambaa

Kitambaa (pia kitambara) ni kipande cha tambaa au jora ambalo kimekatwa ili kushonea vazi la binadamu, kama vile shati, sketi au suruali, au kwa madhumuni mengine, kama vile kutandika meza, kochi au samani nyingine, kushonea pazia, kurembesha, kupenga, kuosha, kupangusa vitu zilizomwagikiwa kiowevu na pia vitu vikavu kama vile madirisha ya glasi n.k.

Kitambaa cha kitamaduni.

Siku hizi vitambaa vinatengenezwa kwa kawaida katika viwanda. Mara nyingi hutengenezwa kwa kuunganisha nyuzi pamoja, ziwe za asili au vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu. Mifano ya nyuzi za asili ni pamba na hariri. Mifano ya nyuzi zilizotengenezwa na binadamu ni nailoni na akriliki[1].

Rangi ya kitambaa inazingatiwa sana katika matumizi, kulingana na utamaduni, hali n.k.

Tanbihi

Marejeo


Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitambaa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.