Lucas Onyango

Lucas Onyango (amezaliwa mnamo 12 Mei 1981) ni mchezaji wa ligi ya raga kutoka Kenya anayeichezea klabu ya Uingereza ya Oldham Roughyeds. Alikuwa mchezaji wa raga wa kitambo wa timu ya taifa ya raga ya Kenya. Yeye ni mchezaji mwenye kasi sana na yeye ni wing'a wakati anacheza.

Lucas Onyango
Personal information
Full nameLucas Onyango
Height179cm
Weight81kg
PositionWing

Nchini Kenya, yeye aliichezea Mean Machine RFC, timu ya Kombe la Kenya ambayo iko chini ya Chuo Kikuu cha Nairobi. Aliichezea timu ya raga ya wachezaji saba kila upande ya Kenya katika Michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka wa 2002 na baadaye yeye alijiunga na Manchester RFC. Alihamia klabu ya ligi raga ya Widnes Waviking mwaka wa 2005.

Dada yake, Sharon Onyango, ameichezea timu ya muungano wa raga ya kitaifa ya wanawake ya Kenya[1]

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Lucas Onyango kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.