Mizungu

Mizungu ni kauli zenye picha na mafumbo zinazoonesha ukinzani wa fikra au tukio.

Mara nyingi mizungu hutumika kwenye hadithi za soga na kwenye mivigha.

Mifano ya mizungu ni:

  • 1. Miti yote nitapanda ila mtalawanda unanishinda - maana yake mpapai.
  • 2. Embe limeiva nyumbani ila nashindwa kulila - maana yake dada au ndugu yangu wa kike.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mizungu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.