Ruhuhu (mto)

(Elekezwa kutoka Mto Ruhuhu)

Mto Ruhuhu ni mto wa Tanzania Kusini. Chanzo chake kiko katika milima ya Kipengere upande wa kusini wa Njombe ikielekea kwanza kusini-mashariki na baadaye magharibi inapoishia katika Ziwa Nyasa karibu na mji wa Manda.

Ruhuhu
ChanzoMilima ya Kipengere, Mkoa wa Iringa, Tanzania
MdomoZiwa Nyasa, upande wa kusini ya Manda (Ludewa)
NchiTanzania
Urefu~300 km

Mwendo wake una urefu wa kilomita zaidi ya 300. Hivyo ni tawimto mrefu wa Ziwa Nyasa na kutokana na hali hii inahesabiwa kama chanzo cha mto Shire unaopeleka maji ya ziwa kwenda mto Zambezi na Bahari Hindi.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje