Mwendamiti

Mwendamiti
Mwendamiti wa Ulaya
Mwendamiti wa Ulaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Faila:Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila:Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli:Aves (Ndege)
Oda:Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu:Certhioidea (Ndege kama tambarazi)
Familia:Sittidae (Ndege walio na mnasaba na wendamiti)
Jenasi:Sitta
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Spishi 20:

  • S. arctica Buturlin, 1907
  • S. azurea Lesson, 1830
  • S. canadensis Linnaeus, 1766
  • S. carolinensis Latham, 1790
  • S. cashmirensis W.E. Brooks, 1871
  • S. castanea Lesson, 1830
  • S. cinnamoventris Blyth, 1842
  • S. europaea Linnaeus, 1758
  • S. formosa Blyth, 1843
  • S. frontalis Swainson, 1820
  • S. himalayensis Jardine & Selby, 1835
  • S. krueperi Pelzeln, 1863
  • S. ledanti Vielliard, 1976
  • S. leucopsis Gould, 1850
  • S. magna R.G.W. Ramsay, 1876
  • S. nagaensis Godwin-Austen, 1874
  • S. neglecta Walden, 1870
  • S. neumayer Michahelles, 1830
  • S. oenochlamys (Sharpe, 1877)
  • S. przewalskii Berezowski & Bianchi, 1891
  • S. pusilla Latham, 1790
  • S. pygmaea Vigors, 1839
  • S. solangiae (Delacour & Jabouille, 1930)
  • S. tephronota Sharpe, 1872
  • S. victoriae Rippon, 1904
  • S. villosa Verreaux, 1865
  • S. whiteheadi Sharpe, 1884
  • S. yunnanensis Ogilvie-Grant, 1900

Wendamiti ni ndege wadogo wa jenasi Sitta katika familia Sittidae. Wana kichwa kikubwa kwa kulinganisha, mkia mfupi na domo na miguu zenye nguvu. Takriban spishi zote zina rangi ya kijivu au buluu juu, nyekundu au nyeupe chini na mstari mweusi machoni. Spishi nyingi zinatokea kanda za wastani za nusudunia ya kaskazini, lakini spishi kadhaa zimejirekebisha na maeneo makavu ya joto. Spishi mbili (mwendamiti wa Atlasi na mwendamiti wa Aljeria) zinatokea Afrika ya Kaskazini.

Wendamiti hula wadudu na invertebrata wengine, hata konokono, na mbegu na makokwa pia hasa wakati wa majira ya baridi. Hulitengeneza tago lao katika tundu mtini au mwanya kwenye mwamba. Jike huyataga mayai 4-10.

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha