Mwokozi

Mwokozi katika teolojia ya Ukristo, ni sifa mojawapo ya Yesu kutokana na imani ya kwamba ndiye aliyetekeleza wokovu wa binadamu wote.

Kristo Mkombozi alivyochorwa na Titian (1534 hivi), Palazzo Pitti, Florence, Italia.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya ·Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Ingawa Injili hazitumii jina hilo, Mtume Paulo alilieneza kupitia nyaraka zake kuhusiana na kifo chake msalabani.[1][2]

Hivyo Agano Jipya linamtaja Yesu Kristo kama Mwokozi mara 16, likisisitiza kuwa ameokoa wote.[3]

Waraka wa kwanza wa Yohane unamtaja kama "kipatanisho cha dhambi zetu, tena si cha dhambi zetu tu, bali cha dhambi za ulimwengu" (1 Yohane 2:2).[4]

Mbali ya Yesu, Agano Jipya linatumia jina hilo kwa Mungu tu (mara 8), wakati Agano la Kale linaita watu mbalimbali kwa jina hilo, kwa sababu ya kuokoa mtu mmoja, wachache au wengi kutoka matatizo mbalimbali.

Tanbihi

Marejeo

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwokozi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.