Panzi

Panzi
Panzi kibyongo, Abisares viridipennis
Panzi kibyongo, Abisares viridipennis
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Faila:Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila:Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli:Insecta (Wadudu)
Nusungeli:Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda:Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda:Caelifera (Panzi)
Ngazi za chini

Oda za chini 2:

  • Acrididea
  • Tridactylidea

Panzi ni aina za wadudu wanaokula mimea. Wameainishwa katika nusuoda Caelifera ya oda Orthoptera. Takriban spishi zote huchupa mbali kwa kutumia miguu yao ya nyuma ambayo ina nguvu sana. Nyingi zinaweza kuruka angani. Panzi wana vipapasio vifupi kuliko mwili wao. Panzi wakubwa ambao wanajikusanya kwenye makundi makubwa huitwa nzige. Kuna panzi wakubwa wengine wenye miiba mikubwa kwenye miguu ya nyuma lakini wasiojikusanya katika makundi. Panzi hao hufanana na ndege wadogo wakiruka juu na huitwa parare.

Panzi majike wana vali mwichoni kwa fumbatio zinazowawezesha kuchimba ndani ya ardhi na kutaga mayai yao katika vibumba. Vibumba vya mayai huweza kuwa na mayai kumi na tano hadi zaidi ya mia moja. Mayai ya spishi nyingi za panzi huingia kwa diaposi kupitia majira ya baridi au kiangazi. Hali ya hewa ikiwa nzuri mayai yaendelea kupevuka halafu tunutu wanatoka. Tunutu (panzi wachanga bila mabawa) hubambua ngozi yao mara tano hadi mara saba kufuatana na spishi. Kila hatua ya ukuaji ni ndefu kuliko ile iliyotangulia. Wakati wa ubambuaji wa mwisho panzi wenye mabawa anatoka na kuwa mpevu ndani ya siku au wiki chache.

Kuna wadudu ambao wanafanana na panzi lakini wana vipapasio virefu kuliko mwili wao. Hawa ni wana wa nusuoda Ensifera. Spishi moja kati yao anaitwa senene na huliwa na watu. Jike ana mrija wa kutaga unaofanana na kitara. Anataga mayai juu ya au ndani ya mimea.

Panzi huliwa sehemu nyingi duniani kwa sababu wana virutubishi vya (protini) vingi. Wanajeshi huambiwa wakamate panzi na kuwala wakipungukiwa chakula.

Mwainisho

Kuna familia nyingi za panzi, lakini takriban spishi zote za Afrika ya Mashariki ni wanafamilia wa Acrididae na Pyrgomorphidae. Mwainisho wa sikuhizi ni kama ufuatao (familia zote hazionyeshwi):

  • Nusuoda Caelifera
    • Oda ya chini Tridactylidea
      • Familia ya juu Tridactyloidea (panzi wachimbaji
        • Familia Cylindrachetidae
        • Familia Ripipterygidae
        • Familia Tridactylidae
    • Oda ya chini Acrididea
      • Familia ya juu Tetrigoidea
        • Familia Tetrigidae
      • Kundi la familia za juu Acridomorpha
        • Familia ya juu Acridoidea
          • Familia Acrididae (panzi wa kawaida, parare na nzige)
          • Familia Dericorythidae
          • Familia Lathiceridae
          • Familia Lentulidae
          • Familia Lithidiidae
          • Familia Ommexechidae
          • Familia Pamphagidae (panzi-chura)
          • Familia Pamphagodidae
          • Familia Pyrgacrididae
          • Familia Romaleidae
          • Familia Tristiridae
        • Familia ya juu Eumastacoidea (panzi-njiti, panzi-kima, panzi-jani)
          • Familia Chorotypidae
          • Familia Episactidae
          • Familia Eumastacidae
          • Familia Euschmidtiidae
          • Familia Mastacideidae
          • Familia Morabidae
          • Familia Thericleidae (panzi vibete)
        • Familia ya juu Pneumoroidea
          • Familia Pneumoridae
        • Familia ya juu Proscopioidea (vijiti warukaji)
          • Familia Proscopiidae
        • Familia ya juu Pyrgomorphoidea (panzi wa rangi nyingi)
          • Familia Pyrgomorphidae (ngeda n.k.)
        • Familia ya juu Tanaoceroidea
          • Familia Tanaoceridae
        • Familia ya juu Trigonopterygoidea
          • Familia Trigonopterygidae
          • Familia Xyronotidae

Familia na nusufamilia za Afrika ya Mashariki

  • Acrididae
    • Acridinae
    • Calliptaminae
    • Catantopinae
    • Coptacrinae
    • Cyrtacanthacridinae
    • Euryphyminae
    • Eyprepocnemidinae
    • Gomphocerinae
    • Hemiacridinae
    • Oedipodinae
    • Oxyinae
    • Spathosterninae
    • Teratodinae
    • Tropidopolinae
  • Dericorythidae
    • Dericorythinae
  • Euschmidtiidae
    • Euschmidtiinae
    • Pseudoschmidtiinae
    • Stenoschmidtiinae
  • Lentulidae
    • Lentulinae
  • Pamphagidae
    • Porthetinae
  • Pneumoridae
  • Pyrgomorphidae
    • Orthacridinae
    • Pyrgomorphinae
  • Thericleidae
    • Afromastacinae
    • Chromothericleinae
    • Plagiotriptinae
    • Thericleinae

Picha