Shist

Shist (pia schist) ni kundi la miamba metamofia iliyotokana na mwambatope na grife.[1]

Shist hii inaonyesha punje ndefu za ulanga.

Mwamba wa shist huwa na punje bapa ndani yake zinazoonekana mara nyingi kuwa na mwelekeo wa sambamba. Shist hufafanuliwa kuwa na asilimia 50 za punje bapa na ndefu[2] kama ulanga, talki au grafati, zinazochanganywa mara nyingi na kwazi na feldspar.[3]

Jina la shist linatokana na Kigiriki σχίζειν (skhízein) inayomaanisha "kupasua",[4] maana miamba ya shist hupasuliwa kwa urahisi kitabaka.

Punje za madini katika miamba ya shist zinaweza kutambulika kwa macho matupu.

Kama miamba mingine ya kimetamofia, shist iliundwa kutokana na miamba yake asilia kwa sababu iliathiriwa na joto na shinikizo kubwa, ingawa si kwa kiwango sawa na miamba ya gneis. Shist ikibaki muda mrefu zaidi chini ya joto na shinikizo inaweza kuendelea kuwa aina ya gneis.

Shist hutofautishwa na kupewa majina mbalimbali kutokana na madini tofauti ndani yake, kama vile garnet schist, tourmaline schist, glaucophane schist, n.k.

Picha

Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shist kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.