Spishi adimu

Shishi adimuni spishi ambazo zimeandikwa na International Union for Conservation of Nature (IUCN) katika orodha maalumu yenye majina ya zile zinazoelekea kukoma duniani (Red List).

Siberian tiger ni spishi iliyo katika hatari ya kutoweka. [1]

Mwaka 2012 orodha hiyo ilikuwa na spishi za wanyama 3079 na spishi za mimea 2655,[2] wakati mwaka 1998 zilikuwa 1102 na 1197 tu.

Inakadiriwa kwamba zaidi ya asilimia 40 za spishi ziko hatarini.

Siku hizi nchi nyingi zina sheria za kuhifadhi spishi za namna hiyo, kwa kukataza, k.mf. uwindaji na uchomaji moto, au kwa kuunda maeneo maalumu hifadhi za taifa.

Pia kuna mikataba ya kimataifa iliyosainiwa na nchi zote au karibu zote kwa ajili hiyo.

Picha

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Spishi adimu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.