Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020 ulifanyika tarehe 28 Oktoba. Wapiga kura walimchagua Rais, wabunge na Madiwani.[1]

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020
Tanzania
2015 ←
28 Oktoba 2020 (2020-10-28)
→ 2025

 
Tundu A. M. Lissu
MgombeaJohn MagufuliTundu Lissu
ChamaChama Cha MapinduziCHADEMA
Mgombea mwenzaSamia SuluhuSalum Mwalimu Juma



President before election

John Magufuli
CCM

Elected President

John Magufuli
CCM

Matokeo ya Uchaguzi wa Rais

Kufuatana na tangazo la Tume la Uchaguzi la 30 Oktoba matokeo yalikuwa kama yafuatayo[2]:

Wapiga kura walioandikishwa walikuwa 29,754,699. Waliopiga kurawalikuwa 15,091,950 (% 50.72), wasiopiga kura walikuwa 14,662,749 (% 49.28).

Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 15,091,950. Kura 261,755 ziliharibika. Jumla ya kura halali ilikuwa 14,830,195.

  • Magufuli alipata kura 12,516,252 (sawa na % 84.40 za kura halali)
  • Lissu alipata kura 1,933,271 (sawa na % 13.04 za kura halali)
  • Wagombea wengine kwa jumla walipata kura 380,672 (sawa na % 2.57 za kura halali)

Wagombea Urais

MgombeaMgombea MwenzaChama
Bernard Kamillius MembeOmar Fakih Hamad [3]Alliance for Change and Transparency (ACT)
Tundu LissuSalum Mwalimu JumaChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Twalib Ibrahim KadegeRamadhan Ali AbdallahUnited People's Democratic Party (UPDP)
Hashim Rungwe SpundaMohammed Massoud RashidChama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)
Leopord Lucas MahonaKhamis Ali HassanNational Reconstruction Alliance (NRA)
John MagufuliSamia SuluhuChama Cha Mapinduzi
Queen Cuthbert SendigaKhamis Juma ShokaAlliance for Democratic Change (ADC)
Muttamwega Bhatt MgaywaSatia Mussa BebwaSauti ya Umma (SAU)
Cecilia Augustino MwangaTabu Mussa JumaDemokrasia Makini
Yeremia Kulwa MaganjaKhamis Haji AmbarNational Convention for Construction and Reform Mageuzi (NCCR Mageuzi)
Prof. Ibrahim Haruna LipumbaHamida Huweishil AbdallaCivic United Front (CUF)
Philipo John FumboZaina Juma KhamisThe Democratic Party (DP)
Seif Maalim SeifRashid Ligania RaiAlliance for Tanzania Farmers Party (AFP)
Khalfan Mohammed MazruiMashavu Alawi HajiThe Union for Multiparty Democracy (UMD)

Yaliyofuata

Baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa kumaliza kutangaza matokeo, vyama vikuu vya upinzani viliungana kukataa matokeo hayo na kudai uchaguzi huru na wa haki chini ya tume huru vikataja kasoro nyingi za mchakato mzima wa uchaguzi[4] [5] [6]

Upande wake Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA) ulizuia mitandao ya kijamii mbalimbali ili kupunguza mawasiliano hasa kutokana na mauaji yaliyotokea Zanzibar.[5]

Nchi na taasisi mbalimbali zimeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu uchaguzi na matokeo yake [7],[8],[9][10].

Tarehe 10 Novemba 2020, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Haki za Binadamu alitoa tamko kuhusu hali tete ya nchi[11] ambalo lilijibiwa mapema na serikali ya Tanzania[12].

Uchaguzi wa 2020 huhesabiwa kuwa ndiyo mbaya kupita yote. Uligubikwa na hila na mbinu chafu. Mbowe alitoa rai yake juu ya uchaguzi huo kwa kusema, ''Kilochofanyika si uchaguzi ni unyang'anyi wa demokrasia uliofanywa na ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) .''[13]

Marejeo