Agatoniki, Zotiki na wenzao

Agatoniki, Zotiki na wenzao (walifariki Silivri, Trakia, leo nchini Uturuki, karne ya 3[1]) walikuwa Wakristo waliofia dini yao hiyo wakati wa dhuluma ya Dola la Roma[2][3].

Kati ya wenzao wanatajwa Teoprepi, Achindini, Severiani, Zenoni, Vikta, Sesarei, Kristofa, Teona na Antonini[4].

Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 21 Agosti[5] au 22 Agosti.

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.