Batilde

Batilde (pia: Bealdhild, Balthild, Bathilda, Bauthieult, Baudour; 627/627 - 680 hivi), alikuwa mke wa mfalme wa Burgundy, Klovis II[1][2], ingawa aliwahi kuuzwa kama mtumwa.

Mt. Batilde.

Hata baada ya kuwa malkia, alibaki mnyenyekevu na kupenda kusaidia maskini na kukomboa watoto watumwa, mbali ya kujenga monasteri mbalimbali chini ya kanuni ya Benedikto wa Nursia na desturi za Wakolumbani wa Luxeuil[3][4]. Alipofiwa mumewe, aliongoza vizuri nchi kwa niaba ya mtoto wake, bado mdogo, na kuzuia biashara ya watumwa.

Miaka ya mwisho aliishi monasterini kwa kufuata kikamilifu sheria za umonaki.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, hasa kisha kutangazwa na Papa Nikolasi I (880)[5].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Januari[6][7].

Tanbihi

Tazama pia

Vyanzo

Marejeo mengine

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN|0-14-051312-4.
  • J.L. Nelson, "Queens as Jezebels: the careers of Brunhild and Balthild in Merovingian history" Medieval Women, D. Baker, ed. (1978) pp 31–77.
  • Alexander Callander Murray, ed. From Roman to Merovingian Gaul: A Reader (in series Readings in Medieval Civilizations and Cultures), 1999. Chapter 14 ""Sanctity and politics in the time of Balthild and her sons"

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.