Wafiadini Wakopti wa Libya

(Elekezwa kutoka Bishoy na wenzake)

Wafiadini Wakopti wa Libya ni Wakristo 20 wa Kikopti kutoka Misri[1] na Matthew Ayariga kutoka Ghana[2][3][4][5][6][7][8] waliotekwa na Waislamu wenye itikadi kali wa Daish huko Sirte, Libya, walipokuwa wanafanya kazi ya ujenzi tarehe 27 Desemba 2014 na mnamo Januari 2015.[9] Matukio ya dhuluma dhidi ya Wamisri nchini Libya yalianza katika miaka ya 1950.[10]

Hatimaye waliuawa kwa kukatwa kichwa kwa ajili ya imani yao[11][12][13][14][15], kama ilivyoonyeshwa katika video tarehe 15 Februari 2015[16]. Kifo chao kilithibishwa na serikali na Kanisa[17].

Tarehe 21 Februari 2015 Patriarki Tawadros II wa Alexandria aliwatangaza kuwa watakatifu[18]. Papa Fransisko amemuomba ruhusa ya kuwaingiza katika Martyrologium Romanum.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifodini chao, 15 Februari.

Majina yao

Ni kama ifuatavyo[19][20][21]:

Bishoy Adel KhalafSamuel Alhoam WilsonHany Abdel-Masih Salib
Melad Mackeen ZakiAbanoub Ayad AttiaEzzat Bushra Nassif
Yousef Shokry YounanKirillos Shukry FawzyMajed Suleiman Shehata
Somali Stéphanos KamelMalak Ibrahim SiniotBishoy Stéphanos Kamel
Mena Fayez AzizGirgis Melad SnioutTawadros Youssef Tawadros
Essam Badr SamirLuke NgatiJaber Mounir Adly
Malak Faraj AbramSameh Salah FaroukMatthew Ayariga

Mwendelezo

Mnamo 19 Aprili 2015, Daish ilisambaza video nyingine iliyoonyesha uuaji wa Wakristo Waethiopia 30 hivi.[22][23][24][25][26][27]

Marejeo

Martin Mosebach aliandika kitabu juu yao: The 21 - A Journey into the Land of Coptic Martyrs.[28]

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.