Charles I wa Uingereza

Charles I (19 Novemba 160030 Januari 1649[1]) alikuwa mfalme wa Uingereza, Uskoti na Ireland kuanzia tarehe 27 Machi 1625 hadi alipouawa.

Charles I alivyochorwa na Anthony van Dyck, 1636

Alishindana na bunge lililotaka kupunguza mamlaka yake, ambayo mwenyewe alifikiri alipewa na Mungu na anaweza kuitumia kadiri ya dhamiri yake.

Alizidi kuchukiwa kwa kuongeza kodi bila kibali cha bunge, kwa kuoa mwanamke Mkatoliki[2] na kwa kuunga mkono wakleri wenye mwelekeo wa Kikatoliki kama vile Richard Montagu na William Laud, pamoja na kujaribu kulazimisha Kanisa la Uskoti kufuata taratibu za lile la Anglikana.

Hatimaye vita vilizuka dhidi yake, kwanza vita vya Maaskofu, halafu tangu mwaka 1642 Charles alipigana na mabunge ya Uingereza na Uskoti katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Aliposhindwa na kusalimu amri mwaka 1645, alikataa sharti la kukubali ufalme wa kikatiba. Kisha kutoroka mnamo Novemba 1647 alifungwa tena katika kisiwa cha Wight.

Hatimaye, chini ya utawala wa Oliver Cromwell, mnamo Januari 1649 alihukumiwa kuwa msaliti na kupewa adhabu ya kifo[3].

Ufalme ulifutwa ikatangazwa jamhuri (Commonwealth of England). Baadaye (1660) ufalme ulirudishwa chini ya mwanae, Charles II wa Uingereza .

Baadhi ya Waanglikana walimuona kama mfiadini na mwaka 1660 walimuingiza katika kalenda ya watakatifu kwa jina la "Mfalme Charles Mfiadini".

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  • 2013  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  •  

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Charles I wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.