Chomboanga

Chomboanga ni chombo cha usafiri chochote kinachoruka juu ya ardhi katika angahewa ya dunia yetu.[1][2][3][4]Vyombo vinvyopita kimo cha kilomita 100 juu ya ardhi huhesabiwa kati ya vyombo vya angani la nje.

Ndege ya kihistoria aina ya Fairey Swordfish

Vyomboanga hupatikana kwa namna mbili:

Zikiwa nyepesi kuliko hewa

  • Puto - ni fuko kubwa lenye ganda la kitambaa au plastiki lisilopenya gesi. Hujazwa gesi nyepesi hasa heli kwa kusidi ya kupazwa hewani. Puto kubwa lina nguvu elezi ya kutosha ya kubeba mizigo kama chumba cha abiria kadhaa.
  • Ndegeputo (au purutangi) ni kama puto kubwa linalobeba behewa kwa abiria au mizigo ikisukumwa na injini kama eropleni.
    • Ndegeputo kubwa zaidi zina chumba kikubwa cha gesi chenye fremu imara inayobeba ganda. Mfano wake ni hasa ndegeputo aina ya Zeppelin zilizosafirisha abiria kati ya Ulaya na Brazil au Marekani kabla ya vita kuu ya pili ya dunia. Baadaye zilipitiwa na ndege kubwa. Hadi leo kuna majaribio ya mara kwa mara ya kuzirudisha kwenye usafiri lakini ni chache tu zinazojengwa.
    • Blimp ni puto kubwa bila fremu ianyohitaji shindikizo la ndani lililo kubwa kuliko shindikizo ya angahewa. Kuna takriban blimpi 30-40 za kibiashara duniani.

Zikiwa nzito kuliko hewa

Picha za Vyomboanga

Marejeo

Viungo vya Nje