Denisi wa Milano

Denisi wa Milano (alifariki Kapadokia, leo nchini Uturuki, 360 hivi) alikuwa Askofu wa 9 au wa 10 wa Milano, Italia Kaskazini katikati ya karne ya 4 (349-355 hivi)[1].

Masalia yake katika kanisa kuu la Milano.

Alimtetea Atanasi wa Aleksandria kwa kulinda imani sahihi dhidi ya Waario na kwa sababu hiyo kaisari Constantius II alimpeleka uhamishoni alipofariki[2][3][4][5].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Mei[6][7].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.