Eklampsia

Eklampsia ni mwanzo wa mitukutiko (misukosuko) katika mwanamke aliye na prekilampsia.[1] Prekilampsia ni ugonjwa wa ujauzito ambapo kuna shinikizo la juu la damu na uwepo wa viwango vikubwa vya protini kwenye mkojo au utendakazi mwingine duni wa viungo.[2][3] Ugonjwa huu unaweza kuanza kabla, wakati wa, au baada ya kujifungua.Mitukutiko ni ya aina ya kitoni na kiklonasi na kwa kawaida hudumu kwa takriban dakika moja. Baada ya mtukutiko, kwa kawaida kipindi cha kuchanganyikiwa au kupoteza ufahamu hufuatia . Matatizo hujumuisha: numonia ya kuvimba mapafu, kuvuja damu kwenye ubongo, kushindwa kwa figo na mshtuko wa moyo. Prekilampsia na eklampsia ni sehemu ya kikundi kikubwa zaidi cha hali zinazojulikana kama magonjwa ya shinikizo la juu la damu katika ujauzito.[1]

Eklampsia
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyObstetrics Edit this on Wikidata
ICD-10O15.
ICD-9642.6
DiseasesDB4068
MedlinePlus000899
eMedicinemed/1905 emerg/796
MeSHD004461

Kinga na matibabu

Mapendekezo ya kinga ni pamoja na: aspirin kwa watu walio katika hatari kubwa, nyongeza ya kalisi katika maeneo yenye upungufu wa kalisi, na matibabu dhidi ya hipatensheni ya awali kwa dawa.[4][5] Mazoezi ya mwili wakati wa ujauzito pia yanaweza kusaidia.[1] Kutumia Salfeti ya magnesiamu ya kudungwa ndani ya mishipa au ndani ya misuli huwasaidia wanawake walio na eklampsia na huwa salama kwa kijumla.[6][7] Hali hii hutokea katika yaliyostawi na mataifa yanayostawi.[6] Huenda mgonjwa akahitaji kusaidiwa kupumua. Mbinu zingine za matibabu zinaweza kujumuisha dawa kama vile hydralazine na kuzaa kwa dharura kupitia ukeni au kuzaa kwa njia ya upasuaji.[1]

Epidemiolojia, prognosisi na historia

Prekilampsia hukadiriwa kuathiri takriban asilimia 5 ya wanawake wanaozaa nayo eklampsia huwaathiri takriban asilimia 1.4 ya wanawake wanaozaa.[8] Katika mataifa yalistawi, viwango vya ugonjwa huu ni takriban mwanamke 1 katika wanawake 2000 wanaozaa, kwa sababu ya uboreshaji wa viwango vya afya.[1] Magonjwa ya shinikizo la juu la damu katika ujauzito ni mojawapo ya visababishi vikuu vya vifo wakati wa ujauzito.[9] Magonjwa haya yalisababisha vifo 29,000 mwaka wa 2013 – vilivyopungua kutoka vifo 37,000 mwaka wa 1990.[10] Takriban asilimia moja ya wanawake walio na eklampsia hufa.[1] Neno eklampsia linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha radi. Maelezo ya kwanza yanayofahamika yalitolewa na Hippocrates katika karne ya 5 BCE.[11]

Marejeo