Eutikyo wa Konstantinopoli

Eutikyo wa Konstantinopoli (Theium, Frigia[1], leo nchini Uturuki, 512 hivi - Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 5 Aprili 582[2]) alikuwa Patriarki wa mji huo kuanzia mwaka 552 hadi 565 halafu tena kutoka mwaka 577 hadi kifo chake kilichompata akiwa anakiri ufufuo wa wafu. Katikati alipelekwa uhamishoni kwa kutetea kwa nguvu imani sahihi[3].

Picha takatifu ya kwake akiwa katika mavazi ya ibada.

Alisimamia Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli (553).

Maandishi yake machache yametufikia[4]

Anaheshimiwa tangu kale kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Aprili[5].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.